Saturday, January 6, 2018

WANANCHI WA BUCHI-BWERA KUPATA DARAJA LA KUDUMU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.Evarist Ndikilo na viongozi wengine wa Mkoa huo wakati wa ziara yake ya kuweka jiwe la msingi katika Daraja la Mbuchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimpa MKandarasi maelekezo juu ya umuhimu wa daraja la Mbuchi kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu kutokana na hali adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo kwa hivi sasa.
Hawa ni wananchi wa kijiji cha Mbwera wakivuka kwa kutumia Mtumbwi kuja kijiji cha Mbuchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali hii ni kutokana na kukosekana kwa daraja linalounganisha vijiji hivyo lakini kwa sasa Ujenzi wa daraja hilo umeanza na utakamilika baada ya mwaka mmoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimskiliza Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibiti kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Mbuchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbuchi na Mbwera kwenye Mkutano wa hadhara wakati alipokuwa anaweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Daraja la Mbuchi.


Nteghenjwa Hosseah,Kibiti.

Wananchi wa Kata ya Mbuchi Tarafa ya Mbwera Wilayani Kibiti kwa kipindi kirefu wametaabika na adha ya kukosa Daraja linalounganisha vijiji hivyo viwili vyevye wakazi zaidi ya elfu 24.

Kukosekana kwa Daraja hilo kumepelekea kukatika kwa mawasiliano ya Uhakika baina ya wananchi wa Mbuchi na wale wa upande wa Pili wa Bwera, kuongeza gharama za maisha na hata kupelekea maafa kwa wakina mama wanaojifungua na wagonjwa kwa sababu ya kukosa njia rahis na nafuu ya kuwafikisha katika huduma za Matibabu.

Vijiji hivyo ambavyo vimetengenishwa na Mto Mberambe ambao ni Tawi la Mto Rufiji na kutengeneza Delta ya Kaskazini tangu kuanzishwa kwake havijawahi kuwa na Daraja la kuwaunganisha katika shughuli zao za kila siku za kila siku za kujiletea Maendeleo.

Wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakitumia Mitumbwi kuwavusha kutoka eneo moja hadi Lingine na huku wakitozwa Tsh 200 kwa safari moja na Pikipiki kutozwa Tsh 1000 kwa safari; Huduma hiyo hupatikana kuanzia saa kumi ba mbili asubuh hadi saa kumi na mbili jioni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani JJafo akiwa ndiye mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa alitembele Tarafa hii miezi kadhaa iliyopita na kuona changamoto hii iliyompelekea kuwaagiza Tarura kuchukua hatua za haraka kwa kujenga Daraja la kudumu litakalounganisha wananchi hao wa maeneo hayo na huduma za kibinadamu.

Na Leo January 05,2018 Waziri Jafo amezuru tena katika vijiji hivyo kukagua Ujenzi wa Daraja la Mbuchi-Mbwera halkadhalika kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi huo utakaotatua changamoto kubwa ya mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wakati wa ukaguzi Daraja hilo Waziri Jafo alisema alitegemea kuona Mkandarasi amepiga hatua lakini ujenzi unaenda polepole sana ukiachilia mbali sababu zilizotolewa na Mkandarasi kuwa wa amechukua muda mrefu kutokana na ubovu wa barabara hivyo imekua ngumu kwake kufikisha materio.

“Nimepita katika barabara hii na nimeona Ubovu wake lakini haya yote ulitakiwa uyafahamu tangu mwanzo wakati unaomba kazi hii, sasa mpaka leo hakuna kazi ya maaa iliyofanyika hapa kama unahisi huwezi bora useme mapema ili tutafute Mkandarasi mwingine mwenye uwezo mkubwa” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa wananchi hawa wamepata tabu kwa kipindi kirefu, wameteseka sana,wamenyanyasika siwezi kuvumilia kuona hali hii inaendelea hawa ni wananchi kama walivyo wananchi wengine wa Nchi hii wana haki sawa wanahitaji huduma muhimu kama Daraja hili liweze kuwaunganisha, katika hili Mkandarasi utaniona mbaya na nitakua narudi mara kwa mara kukagua maendeleo ya ujenzi.

Akielezea maendeleo ya Ujenzi Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibiti amesema ujenzi wa Daraja hilo ulikua uanze Mwezi March,2017 lakini kutokana na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha iliyompelekea Mkandarasi kushindwa kupeleka vifaa na material kwenye eneo la kazi hivyo kuomba tupitia Mkataba na baada ya kufanya hivyo kazi ilianza rasmi mwezi Septemba,2017 na itachukua miezi 15

Daraja hilo ambalo litabadilisha maisha ya wananchi wa Mbuchi-Mbwera litagharimu Tsh Bil 2.4 na litakamilika mwezi Novemba 2018 na linasimamiwa na Wakala wa barabara Wilaya ya Kibiti

No comments: