Sunday, January 28, 2018

WAKULIMA SKIMU YA UMWAGILIAJI MPUNGA NYAMAGOGO MANYONI WALALAMIKIA HALMASHAURI KUTELEKEZA KATAPILA

Na Jumbe Ismailly-Manyoni 

WAKULIMA wa skimu ya umwagiliaji mpunga ya Nyamagogo,iliyopo katika Kijiji cha Chikuyu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuitengeneza katapila lililokuwa likisaidia kusafisha mifereji ya kuoitisha maji kwenye mashamba hayo ili waweze kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambao kwa sasa umepungua.

Mwenyekiti wa skimu hiyo ya umwagiliaji Nyamagogo,Abdallah Rajabu Maganga alisema katapila hilo ambalo limetelekezwa tangu mwaka 2012 kutokana na kukosekana kwa vipuli vinavyohitajika kulifufua kwa sababu kifaa hicho ni aina ya kizamani na hivyo matengenezo yake siyo rahisi na badala yake lingefaa kuuzwa kwa njia yam nada.

“Tatizo wanavyosema sema ni greda la kizamani unaona bwana spea zake hazipatikani sasa tunajiuliza wanaproses kwamba wanataka kuliuza unaona bwana sasa huyo unayemuuzia atalifanyia nini kama kweli ni greda la zamani ambapo hakauna spea”alifafanua Maganga.

Alifafanua mwenyekiti huyo wa (WAUWA) kwamba ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo na kwa sababu sasa hivi dunia ni ya utandawazi spea zinapatikana sehemu yeyote pale hata kama Marekani wanaweza kwenda au kuagiza ili liweze kutengenezwa kwa manufaa ya wakulima hao wa skimu ya umwagiliaji.

Mwenyekiti huyo hata hivyo aliyataja baadhi ya athari wanazopata wakulima hao kuwa ni pamoja na kujaa kwa maji ambayo hupeleka na mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,lakini endapo wangelipata greda hilo lingeweza kuwasaidia kutoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikipotea.

Naye diwani wa kata ya Chikuyu,Benjameni Kamoga alisema kuwa kwa taarifa za awali kutoka Halmashauri zilisema kinachosumbua katapila hilo ni kukosekana kwa cheni ambayo inahitaji nguvu katika matengenezo ili wakulima waweze kunufaika na kuwepo kwa miundombinu hiyo ya kilimo.

“Kwa mfano kuna mikato ambayo imesababishwa na maji kujaa pamoja na ujenzi wa nguzo za umeme,Tanesco walikuja wakatuzibiazibia lakini hawakujua ukubwa, kwa maana hiyo kama lingekuwa zima hili lingetufanyiakazi nzuri”.alibainisha diwani Kamoga.
baadhi ya Skimu za umwagiliaji mashamba ya mpunga Nyamagogo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida yaliyoathirika kutokana na kujaa kwa maji ambayo hupeleka na mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,kwa sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikishuka. 
baadhi ya mitaro iliyojaa mchanga pamoja na takataka na hivyo kusababisha maji kukosa mwelekeo na hivyo kusambaa ovyo kwenye maeneo mengine.
Katapila lililokuwa likiwasaidia wakulima wa skimu ya umwagiliaji mpanga Nyamagogo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida kutojaa kwa maji ambayo hupeleka mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,kwa sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikishuka.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

No comments: