KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) linatarajia kufunga na kuomba kwa muda wa siku 21 nchini kote kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mihili mitatu ya Serikali kuanzia Jumatatu ijayo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt Barnabas Mtokambali wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Biblia (Western Bible College) kilichojengwa Wilayani Uyui na Uzinduzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika Manispaa ya Tabora.
Alisema kuwa kuanzia Jumatatu (22 January 2018) kitakuwa ni kipindi cha kuanza kufunga na maombi ya katika Makanisa ya TAG nchi nzima waumini wake watafunga na kuomba katika maombi yatakayojulikana kama maombi ya Daniel.
Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt .Mtokambali alisema kuwa katika maombi hayo mojawapo ya ajenda ni kumwombea Rais Magufuli na Mihimili yote ya serikali ikiwa ni Serikali, Mahakama na Bunge ili aendelee kuwatumikia Watanzania vizuri kama alivyoanza.
“Mkuu wa Mkoa umeleta ombi lako wakati muafaka la kutaka Kanisa limuombee Rais katika kazi nzuri anazowafanyia Watanzania…Majenerali wa Bwana Yesu wa Kanisa letu wapo hapa kuanzia Jumatau ya tarehe 22 Januari 2018, Makanisa yetu yote tutakusanyika makanisani kwa ajili ya kufunga na kuomba” alisema Askofu Mkuu huyo wa TAG.
“Tutafunga na kuomba kwa siku 21 mfufululizo ambapo maombi hayo yatajulikana kama maombi ya Daniel…ambapo waumini wetu wote watakuwa wakikusanyika kila siku kuanzia saa 10 Makanisani kumwomba Mungu na siku ya Ijumaa tutakesha makanisani..moja ya item ni kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Bunge, Mahakama na Serikali kuu” alisema Dk. Mtokambali.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa uzinduzi wa Chuo na shule hiyo ya Seminari aliwaomba waumini wa TAG na madhehemu mengine hapa nchini kutumia nguvu waliyonayo ya maombi ya kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika kupigania haki mza wanyonge wa nchi hii.
Alisema kuwa maombi hayo yatasaidia kumwongezea nguvu katika mapambano aliyaanza ya kuwakomboa wanyonge dhidi ya watu wachache ambao wamekuwa wakichukua rasimali za nchi hii kwa maslahi binafsi.
Mwanri alisema kuwa wakazi wa Tabora wanaungana na viongozi wa dini katika zote kumwombea na kuongeza Rais asonge mbele wao wako nyuma yake na hawawezi kumuacha pekee yake katika vita hivyo.
No comments:
Post a Comment