Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
TAASISI ya Msichana Initiative imezindua kitabu kidogo kinachozungumzia haki mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike.
Uzinduzi wa kitabu hicho umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa tasisi hiyo Rebeca Gyumi amesema ni vema watanzania wakakitumia kitabu hicho kilichoandaliwa na timu ya mawakili kwani kimeandikwa kwa lugha rahisi zaidi kuhusu maamuzi yote yanayotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Julai 8 mwaka 2016.
“Mahakama Kuu, kupitia Majaji wake katika kesi hii waliona kuwa vifungu hivi haviendani na Katiba ya nchi.Pia vinabagua haki za watoto wa kike ukilinganisha na haki za watoto wa kiume.
"Vifungu hivyo vinaruhusu mtoto wa kiume kuoa katika umri wa miaka 18 na mtoto wa kike kuoelewa katika umri wa miaka 14 na 15 kwa ruhusa ya Mahakama na wazazi,"amesema Gyumi.
Amesema vifungu hivyo vinachochea kwa kiasi kikubwa suala la ndoa za utotoni hasa kwa watoto wa kike na kutaja Tanzania ni moja ya nchi yenye asilimia kubwa ya tatizo la ndoa za utotoni ikilinganishwa na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki ukiacha Uganda.
Ameongeza wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na wasichana hao hukumbwa na changamoto nyingi wanapoingia katika ndoa.
"Wanaolewa wakiwa na mri mdogo wanapopata mimba wakati wa kujifungua wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa sababu via vyao vya uzazi bado ni vichanga.Pia huwanyima haki yao ya kupata elimu,"amesema.
Gymi amesema kupitia kitabu hiki chenye maamuzi ya Mahakama Kuu, jamii itaelewa na kutambua zaidi namna ambavyo vifungu hivyo kandamizi kwa watoto wa kike na kuona haki ambazo zimetambuliwa kisheria kupitia hukumu hiyo, pia madhara ya ndoa za utotoni .
Amefafanua Msichana Initiative pamoja na wadau wengine wanaamini suala la ndoa za utotoni litakoma endapo jamii itakuwa tayari kuwashika mkono watoto wa kike kwa kuwalinda na kutetea haki zao msingi.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya pamoja wageni waalikwa wakiwa wameshika kitabu kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali ya haki za watoto.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali y watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Tamwa, Valerie Msoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika Protea Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria aliyoongoza jopo la Mawakili kupinga sheria ya ndoa za Utotoni katika Mahakama kuu ya Tanzania.
Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Msichana Initiative,Benedict Kikove akitoa neno la shukrani kwa wadau waliofika katika uzinduzi wa kijitabu cha sheria ya kupinga ndoa za utotoni.
Baadhi ya wadau waliofika kushuhudia uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment