Saturday, January 27, 2018

SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 ILI KUIMARAISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface.
.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.



Na WAMJWW. DSM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.

“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za Afya kwa wananchi hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu ya mifupa.

“Niupongeze uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika magonjwa yanayohusiana na mifupa jambo lililosaidia kupunguza wagonjwa wengi sana kupata huduma nje ya nchi” alisema Dkt. Ndugulile.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani Zaidi ya Asilimia 95 ya maradhi ya mifupa hutibiwa katika Hospitali hiyo na asilimia zilizobaki huwapeleka nje ya nchi.

Dkt. Respicious Boniface aliendelea kuishukuru Serikali kwa Msaada huo wa Fedha kwaajili ya kununua Vifaa vya MRI na CT-Scan na kuahidi vifaa hivyo vitafika mapema ndani ya mwezi wa Nne, hivyo kazi ya kuwaudumia wananchi itaanza mapema.

“Sababu kubwa ilikuwa ni vifaa, sasa tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imekwisha toa fedha kwaajili ya vifaa hivyo hivyo ndani ya mwezi wa nne vitakuwa vimekwishafika”, alisema Dkt. Dkt. Respicious Boniface

No comments: