Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Umma kupima
maeneo yao na kuyawekea alama za mipaka ili kuepusha maeneo hayo
kuvamiwa na wananchi.
Waziri Lukuvi amesema hayo mara baada ya kukagua maeneo yaliyo na migogoro ya ardhi katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Aidha
Mheshimiwa Lukuvi akiambata na Naibu wake ambaye ni mbunge wa Jimbo la
Ilemela mkoani Mwanza walitembelea maeneo yaliyovamiwa na wananchi ya
Polisi Kigoto-Kirumba lililovamiwa na wananchi, Uwanja wa Ndege wa
Mwanza na eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Nyamirolerwa katika
manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kutokana
na kujionea uvamizi huo wa maeneo hayo, Waziri Lukuvi amezitaka taazizi
zote za serikali kupima maeneo yao ili wananchi waweze kutambua maeneo
ya Serikali wasiweze kuyavamia jambo ambalo huzaa migogoro.
Hata
hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi waliojenga ndani ya hifadhi ya
Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuondoa maendelezo yao ndani ya siku saba
kabla kuchukuliwa hatua kwakuwa ni wavamizi na hawaruhusiwi kukaa karibu
na eneo linalorusha na kutua vyombo vya anga jambo ambalo ni hatari
kwao na usalama wa vyombo hivyo.
"Hawa
waliojenga ni wavamizi na watambue hivyo majibu tutatoa badaye nini
tutafanya lakini wajue maisha yao siyo ya hapo ndani ya uwanja," alisema
lukuvi.Na
katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi
William Lukuvi amezitaka halmashauri zote nchini kukamilisha zoezi la
ukusanyaji wa kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.
Aliyasema
hayo baada ya kukutana na watumishi na wakuu wa idara wa Manispaa ya
Ilemela na wa jiji la Mwanza wakati wa ziara ya kukagua mifumo ya
ulipaji kodi ya pango la Ardhi na maendeleo ya zoezi la urasimishaji
makazi moani Mwanza.
"Kazi
ya ulipaji kodi sio jambo la hiari ni lazima, kila Mkurugenzi katika
wilaya yake ifikapo Aprili 30, mwaka huu awe ameshja kusanya kodi na
baada ya hapo watakaoshindwa kutekeleza nitatangaza majina yao katika
magazeti ya umma na wataenda kulipia mahakamani, ili malengo yetu
yatimie," amesema Lukuvi
Aidha
Lukuvi amezitaka halmashauri zote kupima viwanja vyote na kuwaagiza
maafisa ardhi kutoa hati kwa wananchi kulingana na majina yao halisia
kama yalivyo katika vitambulisho vya taifa vilivyosajiliwa na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuepusha usumbufu wakati wa
uingizwaji katika mfumo.
Awali
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa zoezi la urasimishaji makazi na
makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi, Mkuu wa Idara ya mipango miji na
ardhi Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando, alisema miongoni mwa
changamoto zinazowakabili ni wananchi kuvamia maeneo yaliyopimwa na
kutengewa Kwa ajili ya matumizi ya umma .
"Kwa
mwaka huu wa fedha hadi kufikia sasa tumekusanya Sh bilioni 1.8 sawa na
asilimia 72 ya lengo la makusanyo ya Sh bilioni 2.5, na jumla ya hati
5,277 Kati ya hati 16,141 zimeandaliwa katika maeneo yaliyorasimishwa
Huku jumla ya viwanja 35,336 tayari vimeingizwa katika mfumo, " alisema.
No comments:
Post a Comment