Saturday, January 6, 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZINDUA UMEME KISIWA CHA FUNDO PEMBA LEO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akibonyeza kitufe kuashiria kuuzindua Umeme katika Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete Pemba ikiwa na shamrashamra za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika kisiwa hicho leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika kisiwa cha Fundo kwa ajili ya Uzinduzi wa Umeme leo mchana.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Maji Ardhi Mazingira na Nishati Mhe. Salama About Talib alipowasili katika Kisiwa cha Fundo kwa ajili ya Uzinduzi wa Umeme.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika Kisiwa cha Fundo kisiwani Pemba ikiwa katika shamra shamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika kisiwa hicho huko Fundo Wilaya ya Wete.(Picha na Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi wa Kisiwa cha Fundo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umeme.(Picha na Ikulu)

WANAFUNZI wa Madrasatul Hidaya Islamia ya Tumbe wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kisiwa cha Fundo kwa ajili ya uzinduzi wa Umeme leo.(Picha na Ikulu)

No comments: