Monday, January 29, 2018

YANGA KUKWEA PIPA ALFAJIRI KESHO KUWAHI MECHI SAA 10 JIONI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Yanga kesho kinatarajia kukwea pipa alfajiri na mapema ili kuwahi mechi yao  dhidi ya Ihefu ikiwa ni mchezo wa kombe la Azam Sports HD  utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine  Jijini Mbeya majira ya saa 10 jioni siku hiyo hiyo.

Timu ya Ihefu inayoshiriki ligi darala la pili ilifanikiwa kuwaondoa timu ya Mbeya City katika mchezo wao wa kwanza huku Yanga wakiwaondoka timu ya Reha na kufanikiwa kuingia hatua ya pili ya kombe la Shirikisho FA .

Yanga itakayoshuka dimbani kesho kuvaana na Ihefu, kikosi chao kinatarajiwab kuondoka alfajiri ya kesho ili kuwahi mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 alasiri huku wakilalamikia ratiba kutokuwa rafiki kwa upande wao.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa timu ya Yanga amesema kuwa kikosi kitaondoka na wachezaji wao wote isipokuwa wale waliokuwa majeruhi ambapo bado hawajaungana na wenzao kikamilifu.

"wachezaji watakaokosekana katika mchezo wa kesho ni saba ambao bado hawajaanza kuungana na wenzao katika mazoezi ya jumla ila wachezaji wengine wote wako katika hali nzuri," amesema Hafidh.

 Hafidh amesema kuwa ratiba ya kombe la FA imekuwa ngumu sana kwao kwani wamekosa hata mda wa kumpuzika kwa wachezaji kwani walichokuwa wanakifahamu kuwa mechi ni Jumatano ila wanakuja kuambiwa kuwa mechi ni Jumanne.

 Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhkweidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 


Michezo mingine itakuwa ni Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.


Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  

Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 


Mchezo kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi Februari 7 wakati mechi nyingine zite zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.

No comments: