Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS
Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya wananchi
wa Dar es Salaam katika mazishi ya aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa
magazeti ya Serikali ya Habari Leo na Daily News Athuman Hamis
yaliyofanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete katika mazishi hayo alikuwa ameongozana na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harson Mwakyembe,
Viongozi wa Serikali, Wahariri, wanaandishi wa habari pamoja na wapiga
picha za habari katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mauti ya mpigapicha huyo yalimkuta jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kabla
ya mazishi hayo, nyumbani kwa marehemu Athumani Hamis Sinza Madukani ,
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya TSN, Dk.Jim Yonas amesema, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda mbali ya kuguswa na kifo cha Athuman
Hamis pia ameahidi kuijengea nyumba familia ya marehemu itakayokuwa na
vyumba vinne.
“Nilikuwa
nazungumza na Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam na ameniambia kuwa
ofisi yake itajenga nyumba ya vyumba vine kwa ajili ya familia ya
marehemu Athuman Hamis,”amesema Dk Yonas.
Pia
amemueleza marehemu Hamis kuwa enzi za uhai wake alikuwa mchapakazi
hodari na licha ya kuwa na matatizo ya kiafya bado aliipenda kazi yake.
Amesema
Athuman Hamis ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari na kuna mengi
ya kujifunza kutoka kwake hasa kwa wapiga picha wa vyombo vya habari
nchini.Akizungumza
baada ya kumzika marehemu Hamis , Imamu wa Msikiti wa Sinza Maijiku
Sheikh Mohamed Suileman amesema enzi za uhai wake Hamis alikuwa ni mcha
Mungu na alipenda kufanya ibada.
Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema Athuman Hamis
wakati wa uhai wake kabla ya kupata kupata matatizo ya ajali alikuwa ni
mtu mwenye kupenda kufanya ibada.
Rais
Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya Kikwete akiweka udongo katika
kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani
Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es
Salaam
Waziri
wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe akiweka
udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya
Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu
jijini Dar es Salaam
Rais
Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri wa
Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe katika
Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Waombolezaji wakihuhifadhi mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Waombolezaji
wakiusaliwa Mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali
Athumani Hamisi katika Msikiti wa Sinza Madukani
Mwenyekiti
wa Chama cha Wapigapicha za Habari nchini, Mwanzo Milinga akiweka
Udongo kwenye kaburi la aliykeuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya
Serikali Athumani Hamisi
Mkurugenzi
wa Mawasiliano Ikulu , Gerson Msigwa akiweka Udongo kwenye Kaburi la
aliyekuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na waombolezaji wengine
nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es
Salaam
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiteta na Katibu wa Chama cha
wapigapicha za Habari nchini Tanzania , Mroki Mroki nyumbani kwa
Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment