Thursday, January 18, 2018

POLISI SHINYANGA YAKAMATA BUNDUKI YA KIVITA AK -47 YENYE SKAFU YA CHADEMA MAJAMBAZI WAKIVAMIA KIWANDA CHA WACHINA

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK-47 iliyotupwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanataka kuvamia kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema walikamata silaha hiyo usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano eneo la Tinde wakati majambazi hao wanafuatiliwa na polisi ndipo wakaamua kutupa bunduki hiyo.

“Silaha hii aina ya AK-47 yenye namba 18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na risasi 25 ndani ya magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa kwenye mfuko mdogo wa nailoni”,alieleza Kamanda Haule.

“Majambazi wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi mbili na koti zito”,aliongeza.

Alisema jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018 kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa Kahama na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha silaha aina ya AK-47 yenye namba 18116428 na mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong 


Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyotelekezwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Wachina mjini Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Silaha na vifaa vilivyotelekezwa na majambazi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha skafu iliyotumika kufunga bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha risasi zilizotelekezwa na majambazi

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF iliyotelekezwa na majambazi

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha koti zito lililotelekezwa na majambazi

Jengo la ofisi za kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),bwana Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi

Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd ,bwana Liu Buhua akilishukuru na kulipongeza jeshi la polisi kuzuia uhalifu katika kiwanda hicho

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments: