Naibu
Waziri wa Madini, Stansalus Nyongo (kulia) akijiandaa kufungua rasmi
Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo wa Buhemba, Wilayani Butiama
Mkoani Mara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) wakati wa kufungua migodi ya
wachimbaji wadogo ya Buhemba. Wa pili kutoka kwake ni Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akijiandaa kufungua rasmi migodi hiyo.
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akifungua rasmi migodi ya
Buhemba ya wachimbaji wadogo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam
Malima akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa migodi ya wachimbaji wadogo ya Buhemba, Mkoani Mara.
Hatimaye
Serikali imefungua Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo iliyopo
katika eneo la Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara baada ya
kujiridhisha hali ya usalama katika migodi hiyo.
Migodi
hiyo imefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
Januari 13, 2018 na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.Akizungumza katika tukio hilo, Nyongo alisema jumla ya migodi 10 imefunguliwa kati ya 16 baada ya kujiridhisha usalama wake.
Alifafanua
kwamba eneo la Buhemba lina jumla ya Migodi ya Dhahabu 16 ambayo
inamilikiwa na Wachimbaji Wadogo hata hivyo iliyokidhi vigezo vya
kiusalama ni Migodi 10 pekee ambayo imeruhusiwa kuendeleza shughuli za
uchimbaji.
Alisema
Serikali ilisitisha shughuli za uchimbaji Madini kwenye eneo hilo la
Buhemba Februari 2017 baada ya kutokea vifo vya Wachimbaji Saba na
wengine wapatao 15 kujeruhiwa kutokana na kufanya shughuli zao bila
kuzingatia taratibu na kanuni za uchimbaji salama.
Alibainisha
kuwa Mwezi Desemba mwaka jana alifanya ziara kwenye eneo hilo ili
kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na
wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao ambapo aliagiza
shughuli za ukaguzi zikamilike ifikapo Mwezi huu wa Januari ili migodi
ifunguliwe.
“Kama
mtakumbuka nilifanya ziara hapa na niliagiza kufikia Januari 10, 2018
Ukaguzi wa Usalama kwenye eneo la Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba uwe
umekamilika ili shughuli za uchimbaji zilizokuwa zimesimamishwa
ziruhusiwe; tumejiridhisha mashimo kumi ni salama na sasa tunafungua
rasmi,” alisema Naibu Waziri Nyongo.Alisema shughuli hiyo
ya Ukaguzi kama alivyokua ameagiza ilifanyika kwa umakini na kwamba
maduara Kumi (Migodi Kumi) yameruhusiwa na mengine Sita hayatoruhusiwa
kuendeleza shughuli za uchimbaji.
Aliongeza
kuwa baada ya kufika kwenye eneo hilo kwa mara ya kwanza alisikitishwa
kuona wananchi wengi wakiwa wamekosa shughuli za kufanya kutokana na
migodi hiyo kufungwa na ndiyo sababu ya kuagiza ukaguzi wake ukamilike
haraka.“Nilivyotembelea hapa Mwezi Desemba mwaka jana
nilisikitishwa kuona shughuli za uchumi kwenye eneo hili la Buhemba
zimesimama kutokana na shughuli za uchimbaji kusimamishwa baada ya
kutokea ajali,” alisema.
Aidha,
Naibu Waziri Nyongo aliwaagiza Wakaguzi wa Migodi kuhakikisha
wanatembelea mara kwa mara maeneo ya migodi ili kukagua hali ya usalama
pamoja na kutoa mafunzo ya uchimbaji salama kwa wachimbaji hususan
wadogo lengo likiwa ni kuepusha ajali.“Ninawaagiza kwa
mara nyingine Wakaguzi wa Migodi kuhakikisha mnatembelea maeneo ya
migodi mara kwa mara ili kuepusha ajali,” aliagiza Naibu Waziri.
Naibu
Waziri Nyongo vilevile aliwaagiza wachimbaji madini kuhakikisha
wanafuata sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji ili kuepusha ajali
migodini na wakati huohuo kunufaika ipasavyo na shughuli zao bila kupata
usumbufu.Aidha, Naibu Waziri alizungumzia ulipaji wa kodi
na tozo mbalimbali ambapo aliwaagiza wachimbaji hao kuhakikisha
wanalipa kwa mujibu wa sheria na alionya kwamba mgodi utakaoshindwa
kulipa inavyostahili, utafungiwa.
“Tumewafungulieni
migodi yenu tukiamini kwamba nanyi mtatimiza wajibu wenu wa kulipa kodi
kwa mujibu wa sheria. Mkishindwa kulipa, hatutosita kuifungia,”
alibainisha Nyongo.Naibu Waziri Nyongo yupo Mkoani Mara kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi na kuzungumza na wachimbaji wadogo.
No comments:
Post a Comment