Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo
nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na wafugaji kuhusu
upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha
kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo
Ndatta)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo
nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo
katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga
chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo
nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji
kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo
huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo
Januari 31.
Dereva
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani
akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi
cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.
Na John Mapepele-Dodoma
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo
nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara
ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini
ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili
jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi
rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua
zaidi baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.
“Wakuu
Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12
jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango
ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa
yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.
Aidha
amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la
kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa nyongeza uliotolewa na
Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.
Akizungumza
katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa
zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya
baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga chapa mifugo
ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa
hatua kali.
Aidha,
Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania
waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa
kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo
la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa
kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali inakadiliwa kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje ya nchi.
Ameutaka
Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali
badala yake kuongeza ushirikiano na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa
ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Awali
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la
upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima
mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana aliongeza siku 30 kwa halmashauri
zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua
nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo
kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo kali.
Alida
kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizosababisha zoezi
hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji
wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri
ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa
majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
Siku
kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina
alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu
tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina
alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe
10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni
ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa Desemba 31
Mwaka jana .
Aidha
alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao
ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya
Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4
kifungu cha 26.
No comments:
Post a Comment