Mkurugenzi
wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) akimuonesha Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi Chumba cha kurushia matangazo wakati wa ziara yake ikiwa ni
sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona
utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati
Jeupe) wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa
kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo
Mjini Dodoma.
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Vyombo
vya Habari nchini vimeaswa kuunga mkono juhudi za Serikali katika
utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza
Wakati wa ziara yake yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi
ya Taifa letu imejengwa katika uchumi jumuishi.
“
Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kueleza faida
za miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli
ya Kisasa (Standard Gauge) kwa wananchi ili nao washiriki kikamilifu
katika utekelezaji wake ambapo ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa
cha maendeleo” Alisisitza Dkt. AbbasiMkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake yake
ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili
kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi akimkabidhi Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura
(Mwenyeshati Jeupe) toleo Maalum la Jarida la Nchi Yetu kuhusu mafaniko
ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah
Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya
utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi
wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma
Akifafanua
amesema kuwa dhamira yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea
kutekelezwa kupitia mfumo wa elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha,
Ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli
na upatikanaji wa huduma muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza
bajeti ili kuhakiksha kuwa kila mwananchi anapata huduma muhimu na za
msingi katika ubora unaotakiwa.
Aliongeza
kuwa Serikali kwa sasa imeweka msukumo na kipaumbele katika kutoa
huduma bora kwa wananchi wote hali inayotoa changamoto kwa vyombo vya
habari kushiriki kikamilifu katika kusaidia juhudi hizo ili malengo yake
yafikiwe kwa wakati.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ABM FM
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa na Mkurugenzi wa RASI FM Bw. Ramadhani Mkosola (kushoto)
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake
yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari
ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini DodomaMkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha RASI FM wakati
wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya
habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.
Katika
kutekeleza majukumu yake Dkt. Abbasi amepongeza vyombo vya habari kwa
kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta
mageuzi ya kweli.Aidha
Dkt. Abbasi aliviasa vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika
kutekeleza majukumu yake ya kila siku ili kuchochea ukuaji wa uchumi na
ujenzi wa Tanzania mpya kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya
Tano.
Ziara
ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali
katika vyombo vya Habari Mkoani Dodoma ni sehemu ya utaratbu
wakutembelea wadau wa sekta ya Habari ili kuimarisha utendaji kazi,
ambapo Leo ametembelea vituo vya redio vya ABM fm na RAS fm.
No comments:
Post a Comment