Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Sophia Mjema amefanya ziara ya kukagua ukarabati wa majengo unaofanyika kwenye Sekondari ya Wasichana Jangwani na Sekondari ya Wavulana Azania ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 3.
Amefafanua kiasi hicho cha fedha pia kinahusisha ukarabati wa sekodari ya Pugu na unafanywa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania(TBA).
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, akiwa Jangwani ambayo alisoma kidato cha tano na sita, Mjema amesema amefanya ziara hiyo kuangalia maendeleo ya ukarabati huo.
"Nitumie nafasi hii kuwapongeza Wakala wa Majengo kwa kazi nzuri wanayoifanya.Pia naomba ukarabati huu uende kwa haraka kama ambavyo imeagizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,"amesema.
Amefafanua ukarabati huo umeleta mabadiliko makubwa katika shule hiyo hasa walipokarabati vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu ambavyo hapo awali havikuwepo Jangwani.
"Kwa ukarabati huu hata wanafunzi wenye uhitaji maalumu wanaweza kuendana na mazingira ya shule kwani yatakuwa rafiki kwao,"amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua Milango ya Choo cha Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani ambayo inakarabatiwa katika mpango maalum wa ulitolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk John Magufuli ya ukarabati wa shule kongwe ambapo ukarabati huo umegharimu Shilingi Bilioni 3 za kitanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akikagua Mabweni ya Shule Sekondari ya Wavulana ya Azania ambayo inakarabatiwa na Wakala wa Majengo TBA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akizungumza na Wasichana wa shule ya Sekondari ya jangwani juu ya kujiepusha ngono wakiwa shuleni ili wasipate Mimba.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akisalimiana na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Azania Sekondari Goodlove Kapufi kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa ukarabati wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua mazingira ya shule ya sekondari ya Jangwani,Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo
Wanafunzi wa Sekondari ya wavulana Azania wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akiwa ameketi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani
No comments:
Post a Comment