Wauzaji
wadogo wa mbole Mkoani Rukwa wamesifu juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuhakikisha wakulima wanapatiwa mbolea kwa wakati na kwa bei
elekezi inayoendana na maeneo husika ambayo mbolea hiyo inasambazwa
kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata hadi Vitongoji.
“Tunashkuru
kwamba zile bei elekezi za mara ya kwanza nina imani hawakujua
Jiografia ya Mkoa wetu, lakini kwa sasa hivi hizi bei ambazo
wametuelekeza zitawasaidia wananchi na sisi tupo tayari kupelekea sehemu
yoyote na faida tutaipata, serikali imetutendea haki,” Damas Kofiambili
mmoja wa wafanyabiashara wadogo wa mbolea alisema.
Sifa
hizo zimeibuka baada ya Uongozi wa Serikali ya mkoa wa Rukwa kutangaza
bei elekezi mpya zilizopitishwa na kamati za pembejeo za wilaya kufuatia
maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mh. Charles Tizeba wakati
akikagua maghala ya mbolea Jijini Dar es Salaam ambapo alizitaka kamati
hizo kufanya marekebisho ya bei hizo ili kuendana na gharama halisi za
usafirishaji ili mbolea iweze kumfikia Mkulima hadi ngazi ya Kijiji.
Akisoma
bei hizo mpya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya
amesema kuwa bei hizo zilizopangwa zimezingatia maoni ya wafanyabiashara
na wadau wa kilimo pamoja na kuandaa fomu maalum zitakazotumika katika
ngazi ya kata ili kuweza kujua kiasi cha mbolea kilichoingia kila siku
katika ngazi ya kata na kumfikia mkulima kwa bei hiyo elekezi.
“Kwa
makao makuu ya Wilaya ya Kalambo Bei ya DAP imepanda kutoka 57,165 hadi
58,022 na maeneo ya kata na vijiji ni 62,522 na UREA imepanda kutoka
44,711 hadi 45,443 na maeneo ya vijiji ni 49,943. Kwa makao makuu ya
Wilaya ya Nkasi Bei ya DAP imepanda kutoka 56,018 hadi 57,000 na maeneo
ya kata na vijiji ni 60,000 na UREA imepanda kutoka 43,565 hadi 44,000
na maeneo ya vijiji ni 47,000.
Kwa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Bei ya DAP imebaki vile vile, maeneo ya kata na vijiji ni 62,000 na UREA imepanda kutoka 44,480 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 49,500. Kwa makao makuu ya Manispaa ya Sumbawanga Bei ya DAP imepanda kutoka 55,442 hadi 56,000 na maeneo ya kata na vijiji ni 57,000 na UREA imepanda kutoka 42,989 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 46,000,” Alimalizia.
Kwa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Bei ya DAP imebaki vile vile, maeneo ya kata na vijiji ni 62,000 na UREA imepanda kutoka 44,480 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 49,500. Kwa makao makuu ya Manispaa ya Sumbawanga Bei ya DAP imepanda kutoka 55,442 hadi 56,000 na maeneo ya kata na vijiji ni 57,000 na UREA imepanda kutoka 42,989 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 46,000,” Alimalizia.
Marekebisho
hayo yamefanywa kwa mujibu wa kanuni ya 56 (4) kwa Mamlaka ya Mbolea
nchini (TFRA) kupewa jukumu la kupitia na kurekebisha bei za mbolea
kulingana na sababu maalum. Hivyo wadau na wafanyabiashara wote wa
mbolea Mkoani Rukwa wametakiwa kutumia bei hizi mpya zilizopitishwa na
kamati za pembejeo za Wilaya.
Hayo
yote yamejiri baada ya Rais John Pombe Magufuli kutoa agizo la
kusambaza mbolea kwa mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji nchini baada ya
kusikia mikoa hiyo bado inasuasua katika upatikanaji wa mbolea hasa
katika msimu huu wa kilimo. Hivyo hadi sasa Mkoa unahitaji tani 2618 za
mbolea ya kupandia (DAP) na tani 6958.6 za mbolea ya kukuzia (UREA).
No comments:
Post a Comment