Wednesday, December 20, 2017

Ziara ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu akiendelea na ziara ya kikazi, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis (aliesimama) akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (hayupo pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko la Bandari Bubu ndani ya Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu. Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara itupatie gari la kufanyia doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake Kamishna Sururu katika ziara yake hiyo ya kikazi Mkoani humo, aliahidi kulifanyia kazi ombi mapema iwezekanavyo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali. Wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akikagua kitabu cha utoaji wa Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi. Huku akiwasisitiza Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo wazingatie vyema Sheria na Taratibu zilizopo ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi. Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Hati za Kusafiria za Dharura ni miongoni mwa Hati mbali mbali za Kusafiria zinazotelewa na Idara ya Uhamiaji Nchini
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19 Disemba, 2017. Aidha, Kamishna Sururu aliwataka watumishi wote kuzingatia maadili ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. “Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote. fuateni Sheria na Taratibu tulizowekewa”. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
Mojawapo ya nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.

No comments: