Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibok
akizungumza katika hafla fupi ya kuagwa kwa wazelendo 47 waliopanda
mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Washiriki katika changamoto ya kupanda Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Ndani na utunzaji wa Mazingira.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza
katika hafla ya kuwaaga washiriki wa changamoto ya upandaji wa mlima
Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na Utunzaji wa
Mazingira.
Mwenyekiti
Mstaafu wa Bodi ya Utalii Tanzania ,Balozi Charles Sanga (kulia) alikua
ni miongoni mwa Wazalendo walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima
Kilimajaro.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara anayeshiriki
zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya 10 sasa akazungumza na
washiriki wa zoezi hilo kabla ya kuianza safari.
Mkuu
wa wilaya ya Rombo ,Agness Hokororo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla ya kuwaaga Wazalendo 47 kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu
wa Wilaya ya Rombo ,Agnes Hokororo akimkabidhi Bendera ya taifa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara kabla ya kuanza kwa
safari hiyo.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara akikabidhi Bendera
kwa Mkuu wa kamandi ya Brigedi ya Magharibi,Brigedia Jenerali Mkumbo
aliyekuwa mkuu wa Msafara wa Wazalendo 47 waloshiriki kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Wazalendo
47 walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika
picha ya pamoja na mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Rombo .Agness Hokororo.
Safari katika siku ya kwanza ya kuelekea kilele cha Uhuru ikaanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali ,Georg Waitara akiongoza.
Kundi la Wanahabri lilikua na kazi ya kuchukua taswira za safari nzima ya kulekea kileleni.
Uzalendo wa kuifikisha Bendera ya Taifa katika kilele cha Uhuru ndio uliongeza morali kwa washiriki ya kuendelea na safari .
Wazalendo walipata mapumziko katika eneo la Nusu njia lijulikanalo kama Kisambioni na baadae kuendelea na safari.
Licha ya kuwepo kwa mvua ,bado safari ya Wazalendo 47 iliendelea.
Wengine walipatiwa msaada pindi walipohitaji ili mradi safari iwe rahisi.
Safari
ya Wazalendo haikuwacha nyuma ,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro ,Betrita Loibook na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete .walitembea licha ya kunyeshwa na
mvua.
Wenye kiu walipata maji na baadae kuendelea na sfari.
Hatimae
safari katika siku ya kwanza kwa Wazalendo 47 kuelekea kilele cha Uhuru
ikakamilika mara baada ya kuwasili kituo cha mapumziko cha Mandara.Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,aliyekuwa katika safari hiyo
No comments:
Post a Comment