Monday, December 4, 2017

WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA UWAJIBIKAJI WENYE TIJA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI

Na Robert Hokororo, Kishapu DC

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda amewakumbusha watumishi wa umma uwajibika wenye tija katika maeneo yao ya kazi huku akisisitiza kila idara ina umuhimu wake.

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mh. Kakunda alisistiza kwa kusema mtumishi anapaswa kuyajua vyema majukumu yake anayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Alisema lazima uthibitishe kuwa unatimiza majukumu yako kwa kutekeleza maagizo yote yanayotolewa pamoja na miongozo yote inayokuwepo, sera, programu za nchi pamoja na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. 

“Mtumishi lazima ujue kila kitu ‘at a finger tip’ kilichopo katika dawati lake, Mkurugenzi nae anapaswa kujua kila kitu kinachohusu Halmashauri yake. Kama mtu hujui makujumu yako ina maana hata ukienda likizo pengo lako halionekani,” alisema.

Aliwakumbusha wahasibu hasa katika utunzaji nyaraka za mahesabu na wagavi kutimiza wajibu wao kwa umakini kuepuka hoja huku akionya atakayezalisha hoja atajibu yeye mwenyewe kama ambavyo sheria ilivyopitshwa mwaka jana na si Halmashauri kama ilivyozoeleka 

Naibu Waziri pia aliwatasisitiza wahandisi waache mazpea ya kukaa ofisini na kusubiri ripo bali watoke wakague miradi wenyewe na kutembea na nyaraka zinazohusu miradi hiyo badala ya kumuachia Afisa Mipango mwenyewe.

Awali akizungumza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela aliwataka watumishi kujenga utaratibu wa kutembelea wananchi kujua kero zao badala ya kukaa ofisini kusubiri wawafuate.

Alisema kuwa lengo la viongozi wa mkoa ni kumkumbusha kila mtumishi kwenye halmashauri yake anafanya kazi kwa weledi na kutekeleza taratibu na sheria za utumishi wa umma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara yake. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa neno wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba akifungua kikao kwa ajili ya Mhheshimiwa Naibu Waziri kuzungumza na watumishi. 
Watumishi wa Halmashauri ya Kishapu na viongozi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
Naibu Waziri TAMISEMI, Mh. George Kakunda akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kishapu.

No comments: