Thursday, December 14, 2017

WAKIMBIZI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUNGULIA SOKO LA BIDHAA ZAO

Mtaalamu wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Ofisi ndogo ya Kibondo akizungumza na Wanawake wakimbizi wa Kambi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juu ya Biashara ya ufumaji wa bidhaa kwa wanawake hao waishio ndani ya kambi hiyo na kupatiwa ujuzi wa kuweza kujiongezea kipato.
Muwezeshaji wa Wanawake wa kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR,Beatrice Emmanuel akitoa maelezo namna kikundi cha wanawake wafumaji wanavyoweza kujiongezea kipato katika familia zao kwa kutengeneza na kuuza bidhaa zao katika soko la pamoja linalojumuisha wakimbizi na Watanzania wanaoishi katika vijiji vya jirani na eneo la kambi ya wakimbizi ya Mtendeli. Pia wageni mbalimbali wanaowatembelea eneo la kambi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo wahisani na wadau mbalimbali. lengo la mradi huu wa ufumaji ni kuwawezesha wanawake kupata ujuzi utaowawezesha kujiongezea kipato ili pindi watakaporejea  nchini mwao kila mwanamke aweze kuwa na shughuli inayoweza kumuingizia kipato
 Afisa Uzalishaji kutoka IRC, Foibe Julius, akitoa maelekezo ya namna ya kusuka vikapu  kwa mmoja wa Mwanamke Mkimbizi anayeishi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma 
Msaidizi Mkuu wa Makazi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli- Lulu Malima akiangalia moja ya Bidhaa zilizofumwa na Wanawake wakimbizi wa kambi hiyo ambao wameweza kuuza na kujiongezea kipato ili kuweza kujikimu katika maisha yao.
Wanawake wanaoishi katika kambi ya Wakaimbizi ya Mtendeli ya Wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma wakipanga bidhaa zao katika hali ya usafi ili kuwawezesha wanunuzikuziona kwa urahisi katika eneo lao na kununua.
Mmoja ya Wanawake kutoka kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko akifuma  kikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
 Wanawakewaishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli wakifuma  vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
 Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Wakifuma  Vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC

No comments: