Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristy Ndikilo ameagiza jeshi la polisi mkoa kuwakamata viongozi wa vikundi 10 vya usimamizi wa Korosho vilivyofanya udanganyifu kwa wanunuzi wa korosho na kufanya wafanyabiashara kutaka kususa Korosho hizo.
Akizungumza wakati wa mkutano na wadau wa korosho wilaya ya Mkuranga, Ndikilo amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya vikundi vya wakulima kuweka mawe na mchanga katika magunia ya korosho ili kupata uzito mkubwa kwa lengo la kumdanganya mnunuzi na vikundi hivyo vinapaswa kutoa maelezo juu ya Korosho wanazozipeleka katika maghala yao.
Amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja kwani kufanya udanganyifu kwa zao la korosho ni kuhujumu uchumi kufuatia zao hilo kuongoza kwa kuleta fedha za kigeni na zao namba moja linaloangaliwa na serikali hivyo haliwezi kuchezewa
Amesema agizo hilo linaenda sambamba na kuwakamata wanunuzi wa korosho walioshinda mnada na kuchelewesha malipo kwa wakulima ndani ya siku 4.
"Sitachelea kumkamata yeyote atakae kwamisha mchakato wa kukuza zao hili katika mkoa wangu, walio na haki yao kulipwa walipwe stahiki zao kwa wakati na kuweza kufanya maendeleo yao.
Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima au wasimamizi wa vikundi Wanauza korosho awali zinakua na ubora wa juu na mnunuzi anapokuja kuchukua baada ya kulipia anakuta ubora umebadilika kutoka ngazi ya juu hadi ngazi ya chini jambo linaloonesha kuna mchezo unaofanywa na viongozi na kufanya korosho ishindwe kupata soko.
Aidha ametangaza kuwa msimu wa korosho unaokuja hakutakuwa na uhifadhi usio rasmi wa korosho na korosho zote zitahifadhiwa katika maghara matatu tu kwa mkoa ili kulinda ubora wa korosho na kudhibiti udanganyifu.
Alisema tabia ya udanganyifu unayofanywa na baadhi ya vikundi ndio chanzo cha wakulima kucheleweshwa mafao yao ili kumpisha mnunuzi kujiridhisha kabla ya kulipia jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wakulima.
"Mtu anaehujumu wakulima wa korosho hao wanahujumu uchumi wa nchi na ni lazima wapambane na mkono wa Serikali kwani Kwa sasa zao la korosho ni miongoni mwa mazao yanayoongoza kukuza pato la taifa"alisema.
Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mkuranga Abdallah Ulega amemuomba mkuu wa mkoa kuwasaidia wakulima ambao wanastahili kupata fedha zao kupatiwa kwa muda ili kuharakisha maendeleo.
Alisema Kupima korosho ndani ya muda mfupi na kubaidi kubadilika kwa ubora ni wazi kuwa kuna jambo ambalo ni muhimu kutafutiwa ufumbuzi.
"Mimi nitashirikiana vizuri kusimamia wakulima kutafuta ufumbuzi wa uharibifu na wizi dhidi ya mazao yao kwani wanaoumia ni wananchi ambao ndo wengi kuliko waharibifu" alisema.
Meneja mkuu wa Chama cha Msingi mkoa wa Pwani (COLLECU) Seif Upara amesema jitihada zaidi zinaendelea kuhakikisha wakulima wanapatiwa elimu zaidi kuhusu mfumo wa Stakabadhi Gharani ili kuboresha usimamizi wa zao hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristy Ndikilo akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Mkuranga na Viongozi wa chama Ushirika juu ya Korosho kuchelewa kulipwa wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza hali halisi ya zao la Korosho.
Meneja wa Coreku, Seif Upallah akizungumza hali ya uendeshaji minada ya Korosho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristy Ndikilo akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga.picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment