Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo,
Dkt. Mary Mashingo(aliyeshika fimbo) akipima kina cha KIsima
kilitengenezwa kienyeji kwa ajili ya kunyweshea mifugo katika eneo la
Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera leo. Waliomzunguka ni wataalam
mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifana Halmashauri ya Missenyi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo,
Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mikono) akiongea na wafugaji wa nchini
Uganda leo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la
Omwaarogwamabaare. Kushoto ni Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini
Tanzania, bwana Richard Tumusiime Kabonero kulia (anayecheka) ni Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Martin
Ruheta.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo,
Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mkono)akimweleza jambo Balozi wa Uganda
nchini Tanzania Mhe.Richard Tumusiime Kabonero (kulia) walipokuwa
katika ziara ya kikazi leo kwenye Mto Kagera katika kijiji cha Kakunyu.
Wengine kushoto kwa Katibu Mkuu ni Dkt. Martin Ruheta Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kulia kwa Balozi ni
Suleiman Ahmed saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo,
Dkt. Mary Mashingo akiwa na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe.
Richard Tumusiime Kabonero (Mwenye suti nyeusi) na kushoto ni Katibu
Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athmani kwenye kikao cha kazi
kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kagera.
Picha na John Mapepele
…………….
Na John Mapepele –Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (0784 441180)
Tanzania
na Uganda leo wamekubaliana kuunda mara moja timu ya pamoja ya
wataalamu wa mifugo itakayokuwa ikifuatilia hali ya mifugo ili kudhibiti
milipuko ya magonjwa hatari ya Mifugo.
Akizungumza
leo mjini Bukoba kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na
Uganda ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi wa
Uganda nchini bwana Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa
karibu baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo
siyo kitu cha hiari bali ni jambo la laziima ili kukabiliana na magonjwa
ya milipuko ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili.
Balozi
Kabonero amesema njia bora ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na
timu ya pamoja ya wataalam watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na
kufanya tathmini kila wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi
kushughulikia peke yake.
“Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero
Akizungumzia
kwa upande wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo
anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amesema ushirikiano
huo utasaidia kuboresha huduma za mifugo baina ya nchi mbili kwa
kuzingatia kuwa taaluma ya udaktari wa mifugo imehuishwa na inadhibitiwa
na bodi za taaluma hiyo kidunia.
Aidha,
amewataka wafugaji wa asili kote nchini wabadili mitazamo ya kutegemea
serikali katika kukuza sekta badala yake washirikiane nayo ili
kuharakisha mapinduzi ya sekta ya mifugo.
“Bado
kuna kazi ya kubwa ya kufanya ili kuikwamua sekta, lakini pia tukiamua
kwa pamoja baina ya serikali na wafugaji nadhani tutakuwa na kipindi
kifupi tu cha kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta hii” aliongeza
Dkt. Mashingo
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Mifugo na Masoko kutoka Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, bwana Victor Mwita anasema kuwa kuimarika kwa minada
itakayosimamiwa kisheria katika mipaka ya nchi ya Tanzania na Uganda
itasaidia kuongeza tija katika sekta ya mifugo hapa nchini.
Aidha,
Dkt. Mashingo alisisitiza kwamba wafugaji wenyewe ndiyo wanaoweza
kuifanya sekta kupiga hatua kwa kuzingatia na kusimamia sheria
mbalimbali za mifugo nchini. Alizitaja baadhi ya sheria ambazo ni
kipaombele kwa wafugaji kuzingatia kwa sasa kuwa ni pamoja na Sheria ya
Magonjwa ya Mifugo namba 17ya mwaka 2003 na Sheria za Nyanda za Malisho
na Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.
Akitolea
mfano wa mafanikio yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt.
Mashingo alisema wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza
kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na
watumiaji wengine wa ardhi.
Aidha
alisema magonjwa kama Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa
yasaidia kuongeza idadi ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia
unachangia kuua 80% ya ndama wanaozaliwa.
Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.
Akitolea
mfano wa mafanikio yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt.
Mashingo alisema wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza
kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na
watumiaji wengine wa ardhi.
Aidha
alisema magonjwa kama Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa
yasaidia kuongeza idadi ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia
unachangia kuua 80% ya ndama wanaozaliwa.
Akichangia
katika kikao hicho Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo nchini(NARCO)
Profesa Philemoni Wambura alisema bado kuna mahitaji makubwa ya mifugo
katika viwanda vya nyama.
“Mahitaji
halisi ya ng’ombe wa kuchinjwa katika viwanda vyetu nchini ni 800 kwa
siku lakini bado hatujaweza kufikia lengo hilo. Tuna kazi ya kufanya “
alisisitiza Profesa Wambura
Kaimu
Mkurugenzi Idara za Huduma za Mifugo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Martin Ruheta amesema ili sekta ya mifugo ifanikiwe lazima uzalishaji wa
malisho uboreshwe malisho yanachangia kwa asilimia 70 hadi 80 kwa
ng’ombe wa maziwa na kwa ng’ombe wa nyama inakwenda mpaka asilmia 90
Katika uzalishaji wa mifugo, hakuna miujiza mingine na ndo maana nchi za
wenzetu kama vile Brazil wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta
hii.
No comments:
Post a Comment