Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya
tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi
wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iitwayo NIPO
TAYARI.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt.
Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya
pili ya kampeni ya NIPO TAYARI itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais,Mhe.
Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini Dodoma.
“Mwongozo huo utasimamia na kutekeleza shughuli zinazohusiana na mazingira na
umelenga katika kutoa maelezo stahiki namna ambavyo vituo vya afya, ikiwemo
ngazi za chini mpaka juu ili maelekezo hayo yaweze kutumika katika upangaji wa
mipango na uandaaji wa bajeti zitakazotumika,” amesema Dkt. Komba.
Aidha Dkt. Komba amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuzingatia usafi wa
mazingira pamoja kutumia vyoo bora ili kuweza kudumisha afya njema kwa
maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi ya Mazingira, Anyitike
Mwakitalima amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwahamisha wananchi kuweza
kutumia vyoo bora na mpaka kufikia Juni 2021 kaya zote nchini ziwe zinatumia
vyoo.
“Kutokana na kulegalega katika baadhi ya maeneo, waligundua kwamba
kisababishi kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na
serikali ingeutumia kusimamia usafi wa mazingira kwahyo kampeni hii itahakikisha
mpaka kufikia 2025 kaya zote zinatumia vyoo vilivyo bora” alisema Bw. Anyitike.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel
Duganga amesema kutokana na kukosekana kwa mwongozo huo unaopima hali ya
maji nchini utendaji wa serikali na wadau ulikuwa ukisuasua, lakini sasa
utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu
sahihi.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika
mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya
Afya uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usafi wa Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Stephen Kiberiti akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Andrew Komba wa pili kutoka
kushoto katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira
katika vituo vya Afya.
Wadau wa masuala ya Afya na Usafi wa mazingira wakifuatilia kwa ukaribu taarifa kutoka kwa mgeni
rasmi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji
na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mipango WATERAN Tanzania Abel Dugango akisoma taarifa fupi kuhusu huduma za maji
na usafi wa mazingira mbele ya Viongozi wa Wizara na Wadau wa Sekta ya Afya, shughuli inayoendelea
jijini Dodoma.
Mratibu wa Kampeni ya kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima akitoa taarifa fupi mbele ya wadau wa Afya katika mkutano wa
ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya
uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa
Mkutano wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya kulia ni
mmoja wa waratibu wa kampeni ya Usafi wa Mazingira.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Bumi Mwamasage akipokea mwongozo wa Taifa wa Huduma za
maji na usafi wa mazingira kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dr. Andrew Komba
ambae pia alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akipokea vipeperushi vilivyoandaliwa
kwaajili ya kutoa elimu kutoka kwa Salome Mtenga.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akiwa na
Wadau wa masuala ya Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na
usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment