Na EmanuelMadafa,Mbeya ,JamiiMojaBlog.
Serikali
inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa inawaondoa vijana kwenye mazingira hatarishi
na kuhimiza ushiriki wao kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi ili kuleta
maendeleo katika ngazi zote.
Imeelezwa
kuwa takribani asilimia 56 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kwa mujibu wa ripoti ya nguvu kazi ya mwaka
2014 .
Akizungumza
jijini Mbeya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji
kanda ya magharibi,Mkurugenzi wa maendeleo ya vijana Ofisi ya Waziri Mkuu
,kazi,Vijana ,ajira na wenye ulemavu Ndugu Jemsi Kujusi amesema serikali mara
baada ya kubaini hali hilo iliamua kutengeneza
viwango vya ufundishaji wa stadi za maisha kwa vijana nje ya shule kwa
kuandaa muongozo sanifu.
Amesema
muongozo huo ulinzinduliwa mwaka 2011 na baada ya hapo iliendelea na jitihada
za kuhakikisha kuwa kunakuwa na wawezeshaji wa kitaifa ambao jukumu lao
linakuwa ni kutoa mafunzo kwa waelimishaji rika katika mikoa yao ili kuwafikia
vijana wengi zaidi kwa ngazi zote.
Mkurugenzi
huyo amesema kazi ya kuwaanda vijana kuwa wawezeshaji kitaifa ilianza Kanda ya
Ziwa mwaka 2015 ambapo serikali
iliendelea na jitihada za kuendeshav mafunzo kwa wawezeshaji kitaifa kutoka
mikoa ya kanda ya kati ,Pwani na mashariki.
Amesema hadi
Agosti 2017 jumla ya wawezeshaji kitaifa 60 walikuwa wamefikiwa ambapo lengo la
serikali ni kuwa na wawezeshaji 78 kwa nchi nzima .
Mkurugenzi
huyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwa kanda ya magharibi ambo ni
,Ruvuma,Kigoma,Songwe,Mbeya,Katavi kuhakikisha kuwa wanatambua kuwa wanajukumu
kubwa kwani serikali kupitia wao inataka kuona vijana wakishiriki kwenye
shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuachana tabia za kukaa vijiweni.
Mkurugenzi
wa
Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye
Ulemavu
Ndugu Jemsi Kujusi akifungua mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji
kitaifa kanda ya Magharibi katika ukumbi wa Hospital ya Rufaa Mbeya
Desemba 13 .
|
Washiriki wa Mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji kitaifa kanda ya Magharibi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu
(hayupo Pichani )Ndugu Jemsi Kujusi katika ukumbi wa Hospital ya Rufaa Mbeya Desemba 13 .
|
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya katika mafunzo hayo Ndugu George Mbigima akizunngumza katika mafunzo hayo
|
Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo.
|
Afisa
Maendeleo ya jamii jiji la Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Mafunzo ya
Stadi za Maisha kwa wawezeshaji kitaifa Kanda ya Magharibi Mkoa wa
Mbeya Ndugu Baraka Mronga akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi
katika mafunzo hayo.;
|
Washiriki wa Mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji kitaifa kanda ya Magharibi katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu Ndugu Jemsi Kujusi Ukumbi wa Hospital ya Rufaa Mbeya. |

No comments:
Post a Comment