Wednesday, December 27, 2017

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu Dar es Salaam akiangalia vitalu vya miche ya miti wakati alipowatembelea wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam wakioneshwa ramani ya Msitu wa Hifadhi Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa tatu kushoto) kuhusiana na“eneo la msitu huo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kisarawe, Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiwemo watumishi wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea eneo kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara jana ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto) akioneshwa eneo la msitu Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.

Picha na Lusungu Helela-MNRT



……………………

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.

Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Misitu Kisarawe, Mathew Mwanuo alisema wilaya hiyo ina misitu minne ya hifadhi ya serikali Kuu ambayo ni Ruvu Kusini, Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi.Alisema msitu wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na watu kutoka maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam.

“Msitu huu ulikuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014. Hata hivyo wavamizi hao waliendelea kuvamia kwa nyakati tofauti hadi mwaka huu,” alisema.

Alisema walianza kuwaondoa mwishoni mwa Agosti mwaka huu, Kamati ya Ulinzi na Usalam ya wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na maofis wa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania walianza kutembelea eneo la msitu kuangalia uvamizi na uharibifu uliofanyika katika Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi ikiwa ni pamoja na kuona ukubwa wa uharibifu na namna ya kutekeleza zoezi.

No comments: