Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na
Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) makao makuu
jijini Dar es Salaam jana . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos
Silayo
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya
Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akizungumza na Watumishi
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kabla ya kumkaribisha
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) kuzungumza
na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dos Santos Silayo
akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga baada ya kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar
es Salaam jana .
Baadhi
ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa
makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati
akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa
makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati
akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu
Helela-MNRTBaadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Lusungu Helela-MNRT
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya
kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala
kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia
Wakala
ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu
mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.Amesema
uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya
misitu iliyo chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na
Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.
Ameyasema
hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam.Amesema
TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana na
kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza
majukumu yake kwa uhuru zaidi.
Wakati
akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu
wa TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati
utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe
kipaumbele.Katika hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.
Amesema
chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake
na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa
sokoni pasipo kujali ubora wake.Amesema
kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora
wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo
imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe hafifu.
‘’
Halafu unaenda kumshindanisha na mtu anayeuza mbao ambazo miti yake
imevunwa ikiwa na miaka 18 haziwezi kushindanishwa ubora kati ya mbao
hizo lazima kiwepo chombo cha kuthibiti kama vile kwenye chakula kuna
TFDA na kwenye bidhaa kuna TBS’’ alisema
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga amemtaka kila mtumishi ahakikishe
anapambana na rushwa kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa TFS Prof. Silayo
kuwahamisha watumishi pale inapotokea fununu kuwa mtumishi fulani
anajihusisha na rushwa hata kama bado haijathibitika kwa vile fununu
hizo haziwezi kuanza tu bila ya kuwa harufu ya mazingira ya kupokea
rushwa yanayotengenezwa.
Amesema
katika suala la ugawaji wa vitalu kuna vitendo vya rushwa vinafanyika
kwani baadhi ya watu wanapewa vibali vya kuvuna kwa muda wa miezi minne
lakini uvunaji ule unaendelea kwa muda wa mwaka mmoja wakati ilitakiwa
kitalu hicho kivunwe kwa muda wa wiki mbili tu.’’ Alisema
‘’Mimi
sikurupuki kwenye maamuzi yangu na sio kwamba nasema nimekuja
kuwatumbua leo lakini nina taarifa nyingi kuhusiana na rushwa
inavyotembea katika ugawaji wa vitalu’’‘’Mtendaji ifanyie kazi taarifa hii ya rushwa ila nikiona mambo hayaendi kama ninavyotarajia nitakuja kivingine. alisisitiza
Katika
hatua nyingine , Naibu Waziri Hasunga ameiagiza TFS iongeze ukusanyaji
wa mapato kwa vile mapato yalipo sasa bado hayatoshelezi na
yaliyokusanywa yatumike vizuri.‘’Taarifa nilizonazo kuna maeneo manne
mapato yanavuja paangalieni hapo mparekebishe ‘’ alisema
Wakati
huo huo, Hasunga ameiagiza TFS ianze kuwekeza katika maeneo ambayo
inaona inaweza kuzalisha zaidi kwa mfano kwenye maporomoko ya Kalambo
ili iweze kuongeza mapato‘’Yale
maporomoko ukikaa Zambia huwezi kuyaona vizuri ila ukikaa Tanzania
unayaona vizuri’ tumieni fursa hiyo baada ya miaka miwili ijayo kinaweza
kikawa kituo kikubwa cha utalii nchini.’’Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo amemhakikishia
Naibu Waziri Hasunga kuwa atatekeleza maagizo yake yote aliyoyatoa kwa
maslahi mapana ya TFS.
No comments:
Post a Comment