Na WAMJW - Dodoma
Madereva
nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti
katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali
pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na
sheria za barabarani.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus
Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua
mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za
barabarani unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda
Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu
wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote
ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote
kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo
nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka
zaidi”Alisema.
Alisema
hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo
kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza
kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia
nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea
mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima
kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi
nne,hivyo ni hatua nzuri.
Hata
hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo
yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo
itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria
inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali
ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali
inatengeneza uchumi wa kati na viwanda kwa kuboresha miundombinu
ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda
miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda
Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na
nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi
wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za
barabarani.
Alitaja
takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba
mwaka 2016 ilikua 639, vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017
kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376, vifo 655
pamoja na majeruhi 1,469.
Naye
Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia Mery Kessy alisema zaidi ya
asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni
asilimia 10 tu nchi hizo zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana
na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema
wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni vijana kati ya miaka miaka
15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha
ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa
kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya
afya.
Kamanda
wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu
aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo
pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini
kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau
mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha
kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini
Dodoma.
ASP
Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama
barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama
barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Marlin
Komba anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini
SACP Fortunatus Musilimu.
Katibu
Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude
aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama
barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama
barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakimsikiliza kwa makini
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu
hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani
nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Kamanda
wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu
katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa
usalama barabarani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama
barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment