Monday, December 4, 2017

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali, Bonnah alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali.
Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mbunge Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars.
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo.
Wachezaji wa Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao.
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli.
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi

No comments: