Kampuni
ya Aggrey&Clifford imetoa msaada wa fedha kusaidia kununua mahitaji
kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Sadeline Health Care
Trust kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Mbali na msaada wa
fedha, imetoa vifaa vya shule na vyakula ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi ambapo pia wafanyakazi wa kampuni
walijitolea muda wao kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao kwa ajili
ya kuwapatia faraja.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Aggrey&Clifford, Martha Majura (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Sadeline Health Care Trust, Sara Kitanda (kushoto) mfano wa hundi ili kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Wanaoshuhudia kutoka wa pili kushoto ni wakurugenzi watendaji wa Aggrey & Clifford, Luke Smit, Tel Akuku na Ryan Goslin.
Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakigawa zawadi na kufurahi na watoto hao.
Baadhi ya watoto wakiwa na furaha baada ya kupatiwa zawadi na kuonyeshwa faraja na upendo.
Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford katika picha ya pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Sadeline.
No comments:
Post a Comment