Wednesday, November 15, 2017

Ziara Ya Katibu Mkuu Wizara Ya Habari Aipongeza Idara Ya Habari (MAELEZO) Kwa Ubunifu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (kushoto) akipata maelekezo toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kulia) wakati alipoitembelea Ofisi za Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus Willium.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus Willium.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Willium (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Susan Mlawi (katikati) alipotembea Ofisi za Idara hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) akisoma Jarida la Nchi Yetu wakati alipofanya ziara katika Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nicholaus Willium na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Willium (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Susan Mlawi katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na Eliphace Marwa- MAELEZO




Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Bi. Suzan Mlawi, amepongeza utendaji kazi na ubunifu unaofanywa na Idara ya Habari- MAELEZO katika kuuhabarisha umma juu ya masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Tano.

Pongezi hizo amezitoa leo wakati alipokutana na uongozi wa Idara ya Habari- MAELEZO katika kikao kazi kilichokifanya mahsusi kufahamu majukumu na changamoto zinazoikabili idara hiyo.

“Nyinyi ni idara muhimu sana na yenye majukumu makubwa sana ya kuisemea na kuitetea serikali hivyo mna jukumu la kufanya kazi kwa weledi, kwa kufuata Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma pamoja na taaluma na miiko ya uandishi wa habari ili muwe mfano kwa wanatasnia ya habari mnaowasimamia” alisema Bi. Mlawi.

Aliitaka Idara ya Habari kuhakikisha wanakuwa na vikao vya mara kwa mara na vyombo vya habari ili kushauriana namna nzuri ya kuendeleza tasnia ya habari lakini pia kukumbushana majukumu na wajibu wao kama wanahabari hasa katika kuzisukuma mbele ajenda mahsusi za serikali ya Awamu ya Tano, kama kujenga Tanzania ya viwanda, kudumisha uzalendo na mapenzi kwa nchi pamoja na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bi. Mlawi ambaye alifuatana na Naibu Katibu wake Bw. Nicolaus Wilium, alisisitiza umuhimu wa idara kuendeleza ubunifu katika mawasiliano yake na umma ili kuwawezesha wananchi wakiwemo wa vijijini kuwa na ufahamu mzuri wa mambo mengi makubwa na mazuri ambayo serikali imefanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbassi alisema ujio wa Katibu Mkuu kwenye idara yake ni faraja kwani unaongeza ari na motisha kwa wafanyakazi kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi.

“Nikuhakikishie ndugu Katibu Mkuu tumefarijika kwa ujio wako na tunaahidi kufanyia kazi yale yote uliyotuelekeza ili idara iweze kutekeleza majukumu yake yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria kwa maslahi mapana ya nchi “ alisema Dkt. Abbassi.

Katibu Mkuu na Naibu wake wako kwenye ziara ya kujitambulisha kwenye baadhi ya taasisi zilizoko chini yao, baada ya kuapishwa kushika nyadhifa zao mapema mwezi uliopita.

No comments: