Sunday, November 26, 2017

VIJANA WASOMI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KULILETEA TAIFA MAENDELEO

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Sanga akitoa mada kwenye kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam jana lenye lengo wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.
Vijana wasomi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakiwa kwenye kongamano hilo.
Muonekano wa ukumbi katika kongamano hilo.
Meza kuu katika kongamano hilo. Kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Philip Sanga, Mgeni rasmi wa Kongamano hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila , Mchungaji John Kanafunzi na Mratibu wa kongamano hilo, Ephraim Mwambapa. 
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu.
Burudani ikiendelea.
Maombi yakifanyika.
Waratibu wa kongamano hilo wakijitambulisha. Kutoka kushoto ni Sarafina Kabwe, Irene Sadock, Michael Mhagama na Yona Kilindu.
Katibu Mkuu wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli, akitoa mada.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephraim Mwambapa akitoa mada katika kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga akihutubia kwenye kongamano hilo.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo,Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na waratibu wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja


Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila amewataka Vijana wasomi na wanataalumu nchini kumsaidia Rais Dk.John Magufuli kuliletea Taifa maendeleo.

Ndabila ametoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwahutubia wasomi wanataaluma katika kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark lenye lengo kwa wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.

"Ninyi wasomi mmesomeshwa kwa ajili ya kuwatumia wananchi na taifa msaidieni Rais wetu John Magufuli kuliletea taifa la Tanzania na kanisa maendeleo kwani hakuna mtu mwingine tunaye mtegemea zaidi yenu" alisema Askofu Ndabila.

Askofu Ndabila aliwataka wasomi hao waende kwa wananchi wakawanoe na kuweza kuwiva kisawasawa ili waendenane na kasi ya maendeleo anayoihitaji Rais Magufuli.

Alisema wasomi ndio kundi pekee linaloweza kuitoa nchi katika hatua moja na kuipeleka katika hatua nyingine ya mbali kimaendeleo na kuwa mambo yao makubwa watakayo yafanya yataweza kuwabadilisha wananchi na nchi ikasonga mbele.

"Wananchi hawahitaji kusikia umahiri wenu wa kuongea kiingereza bali wanataka kuona ni jinsi gani mtafanya kwa vitendo kuwasaidia ili kulipeleka taifa mbele kimaenndeleo" alisema Ndabila.

Askofu Ndabila aliongeza kuwa hivi karibuni hapa nchini ilifika meli kubwa ya kitabibu ambayo ilikuwa na madakatari ambapo walikuwa wakitoa matibabu kwa wagonjwa kazi ambayo hata madaktari wasomi wa hapa nchini wakijipanga wanaweza kuifanya kwa kushirikiana na wadau wengine.

Mtoa mada katika kongamano hilo, Amina Sanga mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema vijana wanapaswa kuwa wabunifu badala ya kusubiri kuajiriwa.Aliwataka vijana kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa kujibizana mambo ambayo hayana tija kwa wao na taifa kwa ujuma badala yake waitumie kutafuta fursa za maendeleo.

"Siku hizi vile vijiwe vya kupiga domo mitaani havipo tena vimehamia kwenye makundi ya mitandaoni huko utakuta vijana tena wasomi wakishindani kujibizana vitu ambavyo havina manufaa kwao na taifa" alisema Sanga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga alisema mabadiliko ya maendeleo yanaanzia kwa mtu mmoja, jamii na hadi taifa na ili kupata mabadiliko hayo yanawategemea wasomi na si mtu mwingine.

Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Mwambapa alisema lengo la kongamano hilo ni kuona jinsi gani wasomi na wanataaluma wataweza kutumia taaluma na usomi wao kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kufanyiwa kazi wakati jamii inachangamoto nyingi.Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizuri kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.

No comments: