Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 24/11/2017 hadi
25/11/2017 limeendesha zaoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa
wananchi wa Songo Songo ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri zaidi ya
masaa mawili kufuata huduma ya vipimo hivyo katika Hospitali ya Kilwa
kivinje.
Kaimu
Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya TPDC inayosimamia uendesheshaji na
utunzaji wa Miundombinu ya Uchakataji na Usafirishaji wa Gesi Asilia
inayoitwa GAS COMPANY (GASCO) Mhandisi Baltazari Mrosso wakati wa
ufungaji wa zoezi hilo ameeleza kuwa ni wajibu wao kama Shirika
kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuboresha
maisha ya Wananchi wa Songo Songo ambao pia ni tegemeo kubwa katika
shughuli zinazofanywa na Shirika kuanzia kwenye uzalishaji wa gesi
visimani, uchakataji kiwandani na usafirishaji.
Diwani
wa Kata ya Songo Songo Mh. Said Mwinyi akifungua rasmi zoezi la upimaji
kwa kukipatiwa huduma ya upimaji wa Shinikizo la Damu kutoka kwa
Daktari Octavian Modest.
“Sisi
kama Shirika la Umma ambalo limewekeza katika Kisiwa hiki katika
shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia tunao wajibu wa
kushirikiana na wananchi pamoja na uongozi wa Songo Songo ili kuboresha
maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kwa lengo la kuboresha maisha ya
wananchi, kuboresha uhusiano na kuendelea vyema na shughuli za
uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia na hivyo leo hii tunahitimisha
zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wa Songo Songo pamoja na kukabidhi
vifaa tiba vya upimaji wa ugonjwa wa Kisukari ambavyo hapo awali
havikuwepo.” Alieleza Kaimu Meneja Mkuu GASCO.
Daktari
wa TPDC, Octavian Modest akimtibu moja ya Wazee wa Kijiji cha Songo
Songo waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa Afya liloratibiwa na
kufadhiliwa na TPDC.
Mhandisi
Mrosso aliongezea kuwa utaratibu huu wa upimaji wa Afya ni endelevu na
utakuwa unafanyika mara kwa mara pamoja na kuchangia kwenye ununuzi wa
vifaa tiba mbavyo vinasabisha usufumbufu kwa wananchi wa Songo Songo
kusafiri baharini kwa mwendo wa zaidi wa masaa mawili kufuata huduma za
vipimo na tiba mbalimbali katika Hospitali ya Kilwa Kivinje pamoja na
hayo alimuomba Mh. Diwani wa Kata ya Songo Songo kushiriki kikamilifu
katika zoezi la kuhamasisha Wananchi kuondoa woga wa kupima afya zao.
Wahudumu wa Afya wakimsaidia Mmoja wa Wazee waliojitokeza kupima afya zao katika Zahanati ya Songo Songo.
Aidha
Mh. Diwani ndugu Mh. Said Mwinyi wa Kata ya Songo Songo ameonyesha
kufurahishwa na kitendo cha TPDC kutekeleza zoezi hilo kwa wananchi wa
Songo Songo ambalo limeonyesha utayari wa TPDC katika kuhakikisha Kijiji
cha Songo Songo kinaimarika katika Sekta ya Afya.
“Kwakweli
TPDC mmetupenda wana Songo Songo kwa kutupatia huduma hii muhimu kwa
ajili ya kujua afya zetu kitendo ambacho kinamuwezesha kila mmoja
kujitambua hali yake, kujikinga na kujitunza na maradhi mbalimbali
pamoja na kupata tiba sahihi kulingana na tatizo lililogundulika kama
hali halisi ilivyo bado tuna upungufu wa vifaa tiba na leo tunshukuru
TPDC kutupatia vifaa vya kupima ugonjwa wa Kisukari ambavyo hatujawahi
kuwa navyo na tunaamini vingine hapo mbeleni mtatuletea ili kuhakikisha
nasi ndugu zenu tunapata huduma bora ya afya” alieleza Mh. Diwani.
Baadhi
ya Wananchi wa Songo Songo wakiwa kwenye foleni ya kusubiri kufanyiwa
vipimo vya magonjwa mbalimbali katika Zahanati ya Kijiji cha Songo Songo
Mkoani Lindi.
Aidha
wakati wa ufunguzi wa huduma hiyo, akieleza nia ya zoezi hilo muhimu
kwa wananchi, Meneja Mawaasiliano wa TPDC, Marie Msellemu amesema upo
umihimu mkubwa wa kila Mtanzania kujua afya yake ili aweze kujikinga na
maradhi mbalimbali, kudhibiti madhara ya maradhi aliyonayo, kuimairisha
afya zetu na kuweza kulitumikia taifa kikamilifu.
“Sisi
kama TPDC tunaona ni wajibu wetu kuhakikisha ndugu zetu wa Songo Songo
ambao eneo lao ndilo gesi iligundulika kwa mara ya kwanza wanapata fursa
ya kupima na kutambua afya zao ili waweze kuwa na nguvu na afya bora na
hivyo kuwawezesha kutekeleza shughuli zao za kila siku na ndio maana
TPDC tumeamua kuendesha zoezi hili muhimu kwa wananchi wa Songo Songo”
Alieleza Bi. Msellemu.
Zoezi
la upimaji wa Afya liliambatana na mashindano ya mpira wa miguu, mpira
wa pete na utoaji wa hundi ya Shilingi 4,613,100 kwa ajili ya ujenzi wa
jengo la Mwalimu wa Shule ya sekondari ya Songo Songo.
No comments:
Post a Comment