Thursday, November 2, 2017

TAFITI ZA KISAYANSI ZIKITUMIKA ZITAPUNGUZA MAGONJWA KWA ASILIMIA 40

Katibu wa Tanzania Health Summit, Rebecca John akizungumza juu ya usajili wa ushiriki wa mkutano wa sekta ya afya utakaofanyika Novema 14 hadi 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam. wengine ni Rais wa Tanzania Healt Summit, Dk. Omary Chillo pamoja na Mwakilishi wa APHFTA, Joseph Mhagama.

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

TAFITI  za kisayansi zikitumika kwa ufasaha  zitasaidia kupunguza magonjwa kwa binadamu kwa asilimia 40. Tafiti hizo ni pamoja na wananchi kupata taarifa za masuala ya afya pamoja na kufuata ushauri wa wataalam juu ya kujiepusha na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na  Rais wa Tanzania Health Summit, Dk. Omary Chillo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya Mkutano wa  Kitaifa  wa Sekta ya Afya nchini utakaofanyika Novema 14 hadi 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Chillo amesema kuwa mkutano huo utajadili changamoto za sekta za afya  nchini pamoja na kuboresha sekta hiyo ili iweze kuhudumia jamii kwa upatikanaji wa huduma bora za afya. Amesema mkutano huo utatoa mapendekezo yanayoonesha suluhisho la mjadala watakayojadili na litaandikwa kwenye kitabu na kusambazwa kwa taasisi za afya na kufuatilia utekelezaji wake.

Mada zitazokuwemo katika mkutano huo ni maendeleo ya huduma za afya, mijadala ya watoa mada  wazoefu wa sekta ya  Afya, kuwasilisha matokeo ya uchaguzi, majadiliano katika vikundi pamoja na kuwa na maonesho ya huduma za bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za afya na mashirika ya umma binafsi,”amesema.

Aidha a amesema kuwa  wanatarajia kupata wadau wa Afya takribani 500 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wataalamu wa Afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa, wachumi, wazambazaji wa vifaa tiba na dawa, wawekezaji katika sekta ya Afya pamoja na wadau wote wa sekta ya Afya.

Amesema watafiti mbalimbali watajadili na kutoa majibu ya tafiti zao kama walizofanya kwa panya kugundua magonjwa ambapo tafiti hizo zikitumika vizuri mtu anauwezo wa  kujikinga na magonjwa kwa asilimia 40.

Nae  Katibu wa Taasisi hiyo, Dk Rebecca John ametoa wito kwa wadau wa afya kutoka Serikalini, mashirika binafsi, hospitali, Asasi zisizo za kiserikali,taasisi za kitaalamu, watengenezaji wa bidhaa za afya, wazambazaji, wawekezaji na washiriki wa maendeleo kushiriki katika mkutano huu.



Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Ni jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha upatikanaji wa afya bora kwa kuunganisha tafiti za kisayansi, ubunifu na sera za afya huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mganga Mkuu wa Seriakali, Profesa Hashim Kambi.

No comments: