Mshauri
wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus
Nyange, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Angelina
Kwinga mbegu ya mihogo inayostahimili ukame katika uzinduzi wa mashamba
darasa ya mbegu hiyo ya mihogo, mahindi aina ya Wema 2109 pamoja na
viazi lishe yalioanzishwa kwa ajili ya wakulima wa vijiji nane katika
wilaya hiyo leo kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kwa kushirikiana OFAB.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Ugalla, Geofrey Magambo akizungumza katika uzinduzi
huo wakati akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Kata hiyo na Kijiji
cha Isongwa.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza katika uzinduzi huo.
Mshauri
wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus
Nyange (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi darasa wa shamba la mahindi
katika Kijiji cha Isongwa kilichopo Kata ya Ugalla Ussoke wilayani
Urambo mkoani Tabora.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akikabidhiwa
mbegu ya mahindi ya Wema na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH,
Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa.
Wananchi wa Kijiji cha Isongwa wakisubiri kupata mafunzo ya upandaji wa mbegu ya mahindi katika shamba darasa.
Mtafiti,
Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani
Morogoro akitoa maelezo kwa wakulima wa Kijiji cha Isongwa jinsi ya
kupanda mahindi aina ya Wema.
Mkulima wa Kijiji cha Isongwa, Malando Malando akiuliza swali.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni akiuliza swali.
Wanawake wakulima wa Kijiji cha Isongwa wakijumuika kwenye uzinduzi huo wakiwa na watoto wao.
Mtafiti,
Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani
Morogoro, akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya
mahindi.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
Mtafiti,
Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani
Morogoro, akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo
yaliyochimbwa.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda
mahindi.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akipanda mahindi.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi, akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi huo.
Mtafiti
wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera,
Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Usisya namna ya
kupanda mbegu ya viazi lishe.
Wakulima wa Kijiji cha Kapiluka wakijiandaa kupanda mbegu ya viazi lishe.
Mtafiti
wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera,
Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Motomoto namna ya
kupanda mbegu ya viazi lishe.
Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora
TAFITI
za kilimo zinazofanywa hapa nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa
Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi
wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi
mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba
darasa kwa wakulima wa vijiji nane vya Isongwa, Ussoke, Usisya,
Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na Songambele.
Alisema
mara nyingi tafiti zilizokuwa zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye
makabati bila ya kuwafikia walengwa na jambo lililofanywa na Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la
Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima
matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri na limefurahiwa na kwa hapa kwetu
ni mara ya kwanza kutokea.
"Tuna
amini kuwa hivi sasa uchumi utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya
na hadi taifa na tutakuwa na chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.
Malunkwi
alisema katika wilaya hiyo walikuwa na changamoto kubwa ya kupata mbegu
bora kwani wakulima wengi walikuwa wakitumia mbegu za zamani
walizozizoea na kujikuta wakipata mazao kiduchu lakini kwa ujio wa mbegu
hizo ni ukombozi mkubwa kwao.
Alitaja
changamoto nyingine ambayo inapaswa kuangaliwa kwa karibu kuwa ni bei
kubwa ya mbegu hiyo ya mahindi ambayo inauzwa shilingi 12,000 kwa kilo
mbili huku kukiwa na debe moja la mahindi linalouzwa shilingi 10,000
ambalo wakulima wamekuwa wakilikimbilia kutokana na bei yake kuwa ya
chini ingawa mazao yake hayana tija.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema
mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia ukame wakati ile
ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na michirizi kahawia huku
zikitoa mavuno mengi.
Alisema
COSTECH katika mkoa huo imetoa kilo 60 za mbegu ya Wema, mihogo 40,000
na viazi lishe 75 ambapo katika wilaya hiyo vijiji nane vimenufaika kwa
ajili ya kutengeneza mashamba darasa ambayo yatatoa mbegu
zitakazosambazwa kwa wakulima katika maeneo mengine.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba alisema hivi
sasa mwajiriwa ni mkulima ambaye analima kilimo chenye tija na si
vinginevyo na kuwa serikali siku zote imekuwa ikihimiza kilimo bora
ambapo aliwataka maofisa ugani kupanga ratiba za kuwafikia wakulima.
Mkuu
wa Wilaya hiyo, Angelina Kwinga aliishukuru COSTECH na OFAB kwa
kutekeleza ahadi ya kuwapelekea mbegu kama walivyo ahidi walipokuwa
wakitoa mafunzo kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment