Wanafunzi waaliomaliza darasa la saba mwaka 2017 wa shule ya msingi ya New Version wakiwa wamembeba mwanafunzi Lawrence Lucian aliyeongoza kwenye matokeo ya Darasa la Saba shuleni hapo.
Shule ya Msingi ya New Version ya Kibaha kwa Mathiasi imefanikiwa kung'aa katika mtihani wa taifa darasa la saba mwaka huu kwa kushika nafasi ya pili kiwilaya, nafasi ya tano kimkoa huku kitaifa ikishika nafasi ya 96 na kuwa na wastani wa 205. 1765.
Shule hiyo ya New Vision kwa mwaka huu imepanda kutoka nafasi ya sita iliyoshika mwaka jana katika mtihani wa taifa wa darasa la saba na kuwa ya pili kiwilaya huku kimkoa ikishika nafasi ya 22 na kuwa ya 702 kitaifa huku ikiwa na wastani wa 163.0714.
Mkurugenzi wa shule hiyo inayotoa elimu yake kwa lugha ya Kiingereza, Andrea Mfuko alisema siri kubwa ya ufauli kwa watoto katika shule hiyo ni mfumo mzuri wa ufundishaji na mazingira ya watoto kujisomea kwa utulivulisema kwani kila Mwalimu anahakikisha kabla ya kuhama topic moja kwenda nyingine ni lazima mtoto awe ameelewa vema, kile alichofundishwa.Amesema mbali na masomo, Wanafunzi wa New vision wanafundishwa kujielewa, kujitambua na kujua wajibu walionao kwa jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya shule hiyo yenye usajili namba PW.01/7/010 ni 'Education brings self actualization' ambayo ina maono ya kutoa elimu bora na kujenga jamii yenye kujitambua ambayo itakuwa ni sehemu muhimu ya kutegemewa na taifa.
Aidha amewaasa wazazi na walezi ili kufanya mtoto aweze kupata ufaulu mzuri wametakiwa kutowabagua watoto katika mgawanyo wa kazi za nyumbani na pia watambue wajibu wao wa kuwafuatilia watoto shuleni hasa pale wanapoona hawaendi vizuri kwani elimu ya mtoto na ufaulu wake unategemea sana jitihada za mzazi na mwalimu, iwapo kila mtu anatambua wajibu wake na kumthamini mwenzake kwa nafasi yake.
Amewasihi wazazi kiwatia moyo watoto kutulia na kusoma kwa badii na kupenda zaidi masomo ya Sayansi.
Mfuko alisema malengo yao makubwa ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.
No comments:
Post a Comment