Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi wa Tanzania, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi
ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo
iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa
kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akizungumza
katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe
kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na
Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la
urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mkimbizi wa Burundi anayeishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma Paul Ndalaizye., akitoa maoni kwa niaba ya wakimbizi wanaoishi
katika kambi hiyo wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na
Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye (hawapo pichani), lengo ikiwa kukagua
zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri
wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo nchini Burundi, Pascal Barandagiye
(kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu,
iliyoko Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma.
Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano na wakimbizi hao,
Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi,
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal
Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao
linavyoendelea.
Serikali ya Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na
mali katika kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini
Tanzania wanarejea nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao.
Haya yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo
kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za
Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi
nchini kwao Burundi.
Tangu zoezi la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa
awamu ya kwanza jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao
Burundi sawa na asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya kwanza.
Aidha, mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948
walijiandikisha kurejea nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na
taratibu ndefu zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR
wakimbizi waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani hawaoni
jitihada zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735 kati ya
33948 wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.
Hali hii inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani
wakimbizi wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe.
Pascal Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari kwaajili ya
kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa huduma muhimu
za kibinadamu.
“zoezi la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari linaenda polepole mno tofauti na
matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linaenda kwa kasi
ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na zoezi hilonkuenda taratibu
Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha na huduma nyingine za
kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi la kurejesha wakimbizi
waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi” alisisitiza Barandagiye.
Akiongea katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na
mtendeli, amewahakikishia wananchi wa kuwa Amani nchini mwao ipo ya
kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili warejee kuenga taifa
lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.
Wakimbizi wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado
wanapenda nchi yao Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto
inayowakabili hadi kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu zinazowachelewesha
kurejeshwa mara tu baada ya kujiandikisha, akiongea kwa niaba ya Wakimbizi
walioko kambi ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65) ambaye amekuwa Mkimbizi
mara Sita kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1972 alisema “ Sisi tulishajiandikisha
Zaidi ya miezi mine sasa ili tuweze kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo
makambi” ameiomba serikali ya Burundi na Tanzania na Shirika la kuhudumia
wakimbizi wakae na kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa kuwarejesha
haraka wenye nia ya kurudi Burundi.
Akitoa taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa
Burundi na Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa
Tanzania, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema
kumekuwa na mwitikio Mkubwa wa wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa
hiari nchini Burundi lakini changamoto imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha
kurejea kwao zinawafanya baadhi yao kuahirisha kurejea kutokana na kusubiri
kwa muda murefu.
Serikali ya Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR
linatakiwa kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na pesa
wakimbizi wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati tayari
wakimbizi wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha kukaa kwa
muda mrefu kwenye vituo vya kuwapokelea.
Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni
amesema serikali ya Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa
kwa mujibu wa makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda kurejea
kwa hiari itashirikiana na UNHCR, nchi ya Burundi ili kufanikisha zoezi hilo.
Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao ya asili ni moja kati ya suluhisho
la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa sharia ya kimataifa ya wakimbizi ya mwaka
1951 na Sheria ya Wakimbizi ya Tanzania yam waka 1998 kifungu Na. 3
Zoezi la kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza kuratibiwa
mara tu baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza
walipo kutana Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka kuwa wakimbizi waliopo Katika
Makambi nchi Tanzania warejee nchini kwao kwani Burundi kuna amani ya
kutosha.
Hadi sasa idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na
waomba hifadhi 26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147 kambi ya
Mtendeli na 66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo katika kambi ya
nduta.
No comments:
Post a Comment