Friday, November 24, 2017

Serikali kutoa muongozo was utoaji tiba kwa hospitality nchini

Na.WAMJW,Ruangwa.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto inatarajia kutoa mwongozo wa utoaji tiba kwenye hospitali zote nchini ili kuwe na mfumo mzuri wa dawa muhimu ili kuepusha madaktari kuagiza dawa ambazo zipo nje ya mfumo wa dawa muhimu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali .

“Kabla ya mwisho wa mwaka tunataka kutoa muongozo huo(Standard Treatment Guidline) kwa sababu imekua changamoto kwani wale wauzaji wakubwa wa dawa wamekua wakizitembelea hospitali kubwa na kuwarubuni wanunue dawa zao ambazo zipo nje ya dawa zetu muhimu”

Kwahiyo muongozo huo itakua kila ugonjwa dawa ya kwanza itakua ipi na kama itashindika dawa itakayofuata dawa ipo na hizo dawa zitaagizwa na kutunzwa na Bohari ya Dawa(MSD).

Hata hivyo Dkt.Ndugulile amewataka watendaji wa hospitali hiyo kuweka utaratibu na mpangilio mzuri na unaohitajikwa wa utunzaji wa dawa kwenye stoo ya madawa iliyopo hospitalini hapo,baada ya kukuta hakuna upangaji mzuri wa dawa na vifaa tiba “mmenithibitishia kwamba dawa zote mnazipata kwa asilimia 90 hivyo ni vyema Mfamasia wa Wilaya kuzipanga dawa hizo vizuri na kuweka kiyoyozi ambacho kitasaidia kutunza dawa kwa muda bila kuharibika”

Alisema hivi sasa nchi haina tatizo la upatikanaji wa dawa kwani bajeti ya dawa hivi sasa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni 260 kwa mwaka huu wa fedha “bajeti hii imekua ikitolewa na Mhe.Rais amekua akizitoa fedha zote,hivyo hatuna shida ya fedha hivyo nasi hatutarajii kuwa na shida ya dawa na dawa tunazokuwa tunazipata zitunzwe vizuri”.

Aidha,amezitaka kamati za afya katika ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali zinafanya kazi ipasavyo kwa kusimamia matumizi mazuri ya dawa.

Kwa upande wa ubora wa huduma za afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali hivyo kumekua na mkakati wa kuwa na ubora wa vituo vya serikali kwa kuwapatia nyota kulingana na ubora uliopo kwenye vituo kwa kuangalia utoaji wa huduma,maabara na sehemu zingine za kutolea huduma.

Kwa upande wa Mfuko wa afya wa jamii(CHF) Dkt.Ndugulile amewapongeza wilaya hiyo kwa kusajili kaya 13,788 kutoka 978 mwaka 2016/2017,ambapo wamewapatia vitambulishovya matibabu wazee 4,000.“hivi sasa Serikali inataka kuwa na bima kwa wote kwani gharama ya matibabu kwa sasa ni kubwa sana hasa na kumekua na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa,hivyo tunataka kuwasaidia wananchi ambao hawawezi kumudu gharama hizo ili anavyokwenda kwenye vituo vyetu asiwaze masuala ya kutoa fedha”alisema Dkt.Ndugulile.

Akisoma ripoti ya Wilaya hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Ernest Ntahuka Alisema Halmashauri hiyo imeweza kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa asilimia 85 kutoka asilimia 60 ya mwaka 2015/2016.Hata hivyo alisema Halmshauri ya Ruangwa kwa mwaka 2017/2017 imetenga shilingi milioni 650 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya na tayari imeshatenga eneo la ujenzi lenye ukubwa wa hekari 60 ambapo ramani ya ujenzi huo tayari imeandaliwa

No comments: