Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Msingi Shinamwendwa (Halmashauri ya Mji Geita) alipokwenda kushiriki kuchmba msingi wa ujenzi wa nyumba pacha ya Walimu shuleni hapo.
Akina mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata za jirani.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya Sekondari.
Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Modest Apolinary kupeleka Wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha na mapato na matumizi ya fedha mbalimbali katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mgusu na Mtaa wa Machinjioni Wilayani Geita.
Mheshimiwa Robert amesema hayo wakati wa ziara yake Halmashauri ya Mji Geita yenye lengo la kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati ambapo baada ya uzinduzi kufanyika wananchi wa mtaa wa machinjioni walimueleza kero ya kutopata taarifa ya mapato na matumizi ya michango wanayochangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda mrefu katika mtaa na kata ya Mgusu.
Akijibu kero hiyo Mkuu wa Mkoa amesema "Kama kuna kiongozi wa mtaa au Kata amekula fedha za wananchi hafai kuwa kiongozi serikali itamchukulia hatua kali za kisheria na atarejesha fedha hizo!, Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika".
Mheshimiwa Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo changamoto nyingi katika maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake ya Mkoa mzima katika Halmashauri ya Mji Geita kwa kutembelea na kushirikiana na wananchi kujenga nyumba pacha ya walimu (Two in one) Shule ya Msingi Shinamwendwa, ujenzi wa kituo cha Zahanati Mtaa wa Nyakato , ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari Mgusu pamoja na kukagua eneo la kujenga Zahanati katika Kata hiyo.
Katika ziara hiyo ya Mkoa mzima Mheshimiwa Gabriel amefanikiwa kutembelea Wilaya zote tano (5) na Halmashauri sita(6) na kufanikiwa kujenga, kutembelea na kuanzisha jumla ya miradi 19 katika Sekta za Afya, Maji na Ujenzi huku akikusanya zaidi ya mifuko 800 ya Saruji, tofali za Block 500, Mbao 50. Haya yote ni matokeo ya kazi aliyoianza ya kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila kijiji ndani ya Mkoa huu lengo kuu likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao pia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Mkoa humu.
Wananchi wote katika maeneo aliyopita kufanya kazi wameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali na kuamua kuunga mkono juhudi hizi kwa kushiriki katika utekelezaji wa miradi kama vile kusoma maji, kubeba mawe, mchanga, kokoto, kuchimba misingi na vijana kujitolea kujenga miradi hii.
Na: Magesa Jumapili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
GEITA
No comments:
Post a Comment