Wednesday, November 15, 2017

PROF KAMBI AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA WADAU WA SEKTA YA AFYA NCHINI

--
 Mganga Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof  Mohamemed Kambi  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la  nne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ambalo lilipata fursa ya kujadili jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya Tanzania.
 Rais wa Kongamano laNne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini, DK Omari Chilo akizungumza kabla ya kumaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la nne la wadau wa sekta hiyo lililofanyika Jijini Dar es Salaam leo.
Kiongozi Mkuu wa  HDIF, David McGinty akizungumza katika Mdahalo wa mabadiliko ya Sayansi Ubunifu na Sera katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya wakati waKongamano la nne la wadau wa Sekta ya Afya nchini

Mratibu wa wa Kongamano la 4 la Sekta ya Afya nchini Dr Peter Maduke akizungumza wakati wa kongamno hilo likiwa linaendelea katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Madaktari waliohudhuria Kongamano la Nne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini
 Meneja wa Tanzania kutoka kampuni ya Sproxil, Ashok Maurya, akimueleza mmoja wa wadau wa Sekta ya Afya namna ya mradi wa huduma ya simu za mkononi katika sekta ya Afya unavyofanya kazi.
 Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka HDIF, Hannah Mwandolomo akitoa ufafanuzi kwa wadau waliofika katika banda la maonesho ya programu hiyo wakati wa Kongamano la nne la wadau wa sekta ya Afya nchini lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa  Mkuu wa programu ya  DTREE International,Erica Layer akizungumza na wadau wanaofadhiliwana mradi wa HDIF wakati wa Kongamano la 4 la sekta ya Afya nchini

No comments: