Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitoa mada kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuhusu kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao katika Mkutano Kazi wa mwaka unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwasilisha mada ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akiwasilisha mada ya kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake nchini wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Watoto Bibi Rose Minja akiwasilisha muhtasari wa utafiti wa Shirika la UNICEF kuhusu vichocheo vya ukatili dhidi ya watoto na mabadiliko chanya Tanzania wakati wa Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka OR TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga wakati wa Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma Bw. Deogratias Rwambo akiwasilisha hoja wakati wa siku ya pili ya Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma kwa lengo la kuamsha ari ya kufanya kazi na kutokomeza ukatili ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha Bibi Janet Mashasi akiuliza swala wakati wa siku ya pili ya Mkutano wa Kazi mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma kwa lengo la kuamsha ari ya kufanya kazi na kutokomeza ukatili ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya zote nchini wakifuatilia mijadala ya kuhuisha ari ya wananchi kuitikia kazi za maendeleo yao na kujenga uelewa kuhusu agenda ya kushiriki katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda wakati wa Mkutano wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
…………
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wameendele kujadili jinsia ya kutekeleza kampeni ya Wizara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii na mbinu mahususi katika kufanikisha utekelezaji wa programu mbalimbali zinazohusiana na maendeleo jumuishi ya jamii zetu.
Mbinu hii ina wawezesha wataalam wa maendeleo ya jamii katika sekta za umma na sekta binafsi kuhusisha wananchi kubainisha rasilimali na uwezo wa kitaalamu katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo na kiuchumi ambayo inalenga kukuza ustawi wa watu wenyewe.
Mpango wa kuamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya Taifa unahitaji umuhimu mkubwa wa takwimu katika kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi na uwekezaji kuanzia ngazi ya Kata mpaka taifa.
Vipaumbele vinavyotakiwa kuzingatiwa katika utekelezaji wa ari ya watu kushiriki miradi ya maendeleo ya jamii ni ushiriki wa wananchi kuanzia hatua za awali, kujenga hamasa ya jamii kujitambua na kujiamani katika kujiletea maendeleo yao, kuhimiza jamii kuelewa haki zao na fursa zilizopo katika mazingira yao kuwa na uwakilishi maalum wa jamii husika kuweza kusushughulikia vikwazo vilivyopo, na kutumia taarifa za kiutafiti.
Uamshaji wa ari unaweza kufikishwa kwa wananchi na kujenga uelewa wa wananchi wanaohusika na mradi huo katika kutoa mchango wa kufanya kazi za kujitolea.
Njia hii ya kuamsha ari ikitekelezwa ipasavyo, na maafisa maendeleo ya jamii wakawezeshwa itachochea kwa kiasi kikubwa kubadili mitazamo ya hasi na kuwa na mitazamo chanya maana watashiriki ipasavyo katika katika shughuli za maendeleo yao kuanzioa ngazi ya kaya, jamii, na hadi Taifa na hivyo kutoa mchango katika kujenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.
Mkutano huu unatarajia kutoka na mapendekezo ya vikundi/ kanda ambayo yataenda kutekelezwa katika mikoa na halmashauri husika ili kupata uelewa wa pamoja na mchango kufkia uchumi wa kati na viwanda sanjari na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimi 50 ifikapo mwaka 2021/2022.
No comments:
Post a Comment