Tuesday, November 21, 2017

MEYA WA JIJI LA TANGA APOKEA VIFAA TIBA KUTOKA KUWAIT

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem (kushoto) akimkabidhi mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina Mustapha Selebosi ,kulia 
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem atia saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili katika uzinduzi wa Kisima 
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza wakati wa uzinduzi huo

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji safi na salama katika Mkoa wa tanga mwisho wa wiki ikiwemo shule ya Old Tanga Secondary School vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi huo














Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji safi na salama mwisho wa wiki katika Mkoa wa tanga ikiwemo shule ya Old Tanga Secondary School vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait nchini unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE”, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina Mustapha Selebosi, walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali.

Aidha Balozi wa Kuwait alitembelea kituo cha afya cha Ngamiani ambapo alimkabidhi Mstahiki Meya wa Tanga mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, mabeseni ambayo ni msaada kutoka taasisi ya Red Crescent ya Kuwait. Akiwa mjini Tanga Balozi Al-Najem alihudhuria mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kheri ya wanawake.

Kwa upande wake Meya wa Tanga aliushukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa msaada huo na akamuomba Balozi wa Kuwait pia aweze kusaidia katika shule za jiji hilo 98 za msingi na 32 za sekondari Rkupata huduma ya visima vya maji.

No comments: