Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu
Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Afya Mh.Ummy Mwalimu, huku
wakitembea mapema leo wakati akiongoza a matembezi ya hisani kwa ajili
ya kusomesha Wauguzi
Wakunga , matembezi hayo ya kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja vya
Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais).
Picha ya pamoja na Washiriki wa Matembezi hayo ya Hisani
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, leo ameshiriki katika Matembezi ya Hisani ya Kilomita Nne na
Nusu yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi
na ukunga.
Akihutubia mamia ya
wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Green Ground- Oysterbay mara baada ya
matembezi hayo, Makamu wa Rais alisema takwimu za vifo vya kina mama
zimeongezeka, hivyo wazo la kusaida kuongeza idadi ya wakunga ambao watasaidia
kupunguza vifo hivyo ni zuri sana.
Makamu wa Rais alisema “nimefarijika
kusikia kuwa mwaka 2016 matembezi haya ya hisani yalikusanya wastani wa
shilingi milioni 290 pesa ambayo iliwekwa katika fungu la kusomesha wauguzi
wakunga wapya 75 katika mafunzo ya ngazi ya cheti” . Makamu wa Rais alionesha
kufurahishwa na malengo yaliyowekwa kwa miaka miwili ijayo ya kukusanya kiasi
cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi 400 katika
ngazi ya cheti na diploma kwas njia ya masafa.
Makamu wa Rais alisisitiza
kuwa moja ya chanzo cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua ni
ukosefu wa wataalam wa kuwahudumia. Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa zaidi
ya asilimia 60 ya akina mama hawaendi kujifungua katika vituo vyetu vya kutolea
huduma kutokana na kukosekana kwa wataalam wa kuwahudumia akina mama hao.
Makamu wa Rais
aliwahakikishia wadau wote wa sekta ya afya kwamba serikali ipo nao bega kwa
bega katika kuhakikisha wanaotaka kuwekeza katika sekta hii wanafanikisha
malengo yao. Aidha, alisema serikali inaendeleza juhudi za kuinua uchumi kwa
kuongeza idadi ya viwanda ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengeneza dawa na
vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za afya kwa
binadamu.
Makamu wa Rais aliiagiza
Wizara ya afya iusimamie kikamilifu mwongozo unaotaka kila kifo cha mama na
mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndani ya saa 24 katika
kituo au hospitali husika kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo hicho na
kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi huduma zinazotolewa
katika kituo husika.
Mwisho,Makamu wa Rais
aliwashukuru wadau ,wahisani na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye
matembezi hayo na kuwaomba kuendelea kushiriki na kuchangia fedha kwa ajili ya
kusomesha wakunga wauguzi.
No comments:
Post a Comment