Waziri
wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizindua Mwongozo wa
Kampeni ya uanzishwaji wa Viwanda kwa kila Mkoa hapa nchini ili kuendana
na dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza ujenzi wa uchumi
wa viwanda.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akisisitiza umuhimu wa
Wakuu wa Mikoa Kusimamia Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda 100 katika
kila Mkoa wakati akizindua kamapeni hiyo leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa Ujenzi wa Viwanda
katika kuzalisha ajira kwa Vijana na kukuza uchumi wa nchi.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akionesha moja ya
viatu vinavyozalishwa hapa nchini katika Viwanda vidogo na vya Kati
wakati akikagua mabanda ya wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali
zikiwemo za ngozi mara baada ya kuzindua kampeni yenye kauli Mbiu ya
“Mkoa Wetu Viwanda vyetu” ili kuhamasisha ujenzi wa Viwanda katika Mikoa
yote nchini.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa(kushoto), kulia ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walioshiriki katika Uzinduzi wa
Kampeni ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati katika kila Mkoa.
( Picha zote na Frank Mvungi – Maelezo, Dodoma)
…………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya
“Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika
kila Mkoa nchini, leo Mjini Dodoma.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mhe. Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili
nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika
viwanda.
“Historia
ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961
Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo
tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa
na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na
Serikali” ameeleza Mhe. Jafo.
Aidha
amesema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi
pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na
Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na
kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.
“TAMISEMI
kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa
uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za
Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya
soko” amefafanua Mhe. Jafo.
Hata
hivyo, Mhe. Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na
Halmashauri kuwatumia ipasavyo Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa
Ugani ili kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa
uchumi wa viwanda nchini.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi
Stella Manyanya amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuweka mazingira
wezeshi ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya
uendelezaji viwanda katika Ofisi zote za SIDO Mikoani.
Naye
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa
wetu viwanda vyetu itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa
vijana nchini.
No comments:
Post a Comment