Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya
pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi
Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi.
Uzeeli Kiangi (katikati) katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema
mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia
kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa
Utalii Domina Moshi (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimkabidhi
moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi
wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli
Kiangi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya
kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa
Sheria ya utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akiwa na Afisa Utalii, Nina Kisando
(katikati) wakiwa wanatabasamu huku wakionesha moja ya zawadi ya saa ya
mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai
mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi
Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi.
Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria
ya Utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akikata keki katika katika hafla ya kustaafu
kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma tayari kuwalisha Watumishi
wa Wizara. Kushoto kwake ni Marygoreth Mushin a Kulia kwake ni Mary Msekela.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akimlisha keki Afisa Utalii Mwandamizi
ikiwa ni ishara ya kuagana katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria
ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,
Bw. Deograsius Mdamu.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi ( wa pili kushoto) akisindikizwa na baadhi
ya Watumishi wa Idara ya Utalii mara baada ya hafla ya kustaafu kwake kwa
Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii
katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi ( wa pili kushoto) akiwa na Afisa Utalii,
Dorothy Mtweve mara baada ya hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria
ya Utumishi wa Umma kumalizika.( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
No comments:
Post a Comment