Na David John
MWENYEKITI wa Shirikisho la Waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdallahaman Lutenga Amesema chini ya uongozi wake atahakikisha hakuna fisadi wala mchwa yeyote atakaengia kwenye shirikisho hilo.
Amesema kuwa wanachama wa shirikisho hilo lazima watambue kuwa shirikisho hilo ni mahala patakatifu na viongozi wanaokwenda kuongoza shirikisho lazima wawe waadilifu na wenye uchungu na si vinginevyo.
Lutenga ametoa kauli hii mapema leo katika mahojiano maalum ambapo alikuwa anajibu hoja mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa shirikisho hilo.
Amesema kuwa anasikia malalamiko na hoja ambazo zinatolewa na baadhi ya waganga hususani wakihoji uhalali wa yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti ambapo amesema yeye yupo kwa mujibu wa Katiba yao na Kama kuna watu hawataki basi wanaweza kwenda Mahakamani.
Mwenyekiti huyo taifa amesema kuwa yeye ataendelea kuwa mwenyekiti hadi uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakapofanyika mwishoni mwa 2018 nakudai kuwa wajumbe wa halmashauri kuu kwa mujibu wa katiba yao kwa Kauli moja waliwaongezea muda ili kukamilisha baadhi ya mambo.
"Nataka nikuambie ndugu mwandishi unajuwa kuna watu wachache wanaleta vurugu ili uonekane kuna mgogoro ndani ya shirikisho lakini kikubwa watu hawasomi katiba inaelekeza nini. "amesema Lutenga
Nakuongeza kuwa kama kuna watu wanataka uongozi wasubili hadi muda utakapofikat.nakwamba hata hivyo muda ukifika chini ya uongozi wake hakuna majizi wala mafisadi watakaopewa nafasi ya kuingia kwenye uchaguzi huo.
Lutenga amesema anawasikia baadhi ya wanachama kuhoji kwanini yeye anakwenda mikoani kufanya kazi za shirikisho lakini wanasahau kama mimi ndio msemaji wa shirikisho hilo na ndio anateua viongozi wa mikoa na Wilaya kwa mujibu wa katiba yao
"Sikiliza nikuambia Mwandishi hawa watu wanamatatizo na tatizo kubwa hawasomi katiba yetu hivyo ninachofanya kupo ndani ya katiba. Narudia tena hakuna dili wala rushwa hapa. na wote ambao wanakwenda kinyume na taratibu zetu sitawaonea haya. "amasema Lutenga.
Lutenga ametoa rai kwa wanachama wake kuendelea kuheshimu katiba na kama kuna watu wanadhan yeye anavunja katiba basi wasikae kupiga majungu bali waende Mahakama lakini si kupiga kelele kwenye miitandao na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment