Sunday, November 5, 2017

DC KIBONDO AWAAGIZA MADIWANI KUHAMASISHA WANANCHI KUIBUA VITUO VYA AFYA KATIKA KATA ZAO.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WILAYA ya Kibondo inakabiliwa na upungufu wa vituo vya Afya, ambapo katika Wilaya nzima kuna vituo vya afya viwili hali inayopelekea Wananchi wa Wilaya ya Kibondo kukosa vituo vya kwenda kutibiwa na kupelekea ongezeko la vifo kwa Wananchi kutokana na kukosa huduma.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura amewaagiza Madiwani kuhakikisha wanawahamasisha Wananchi katika kata zao kuibua vituo vya Afya kwa kuanzisha ujenzi Wa vituo hivyo na Halmashauri kumalizia ujenzi huo ili kuhakikisha vituo vya Afya katika Wilaya hiyo vinaongezeka.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Juzi Mkuu huyo alisema jambo la aibu sana kwa Wilaya hiyo kuwa na vituo vya Afya viwili na halmashauri isipochukua hatua ya kurekebisha vituo hivyo vitarudi kuwa zahanati, na amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuhakikisha anaongeza mbinu ya kuibua vituo hivyo angalau Wilaya hiyo kuwa na vituo 10 kwa kuanzia.

Aidha Bura alisisitiza Madiwani kupatiwa Vitambulisho vya bima ya afya ili na wao waweze kuwahamasisha wananchi kuchangia mfuko wa bima ya Afya (CHF) na waweze kupatiwa matibabu bure na kupunguza gharama za matibabu.

"Halmashauri inatakiwa kuingiza bajeti ya vituo vilivyo ibuliwa na kuanza kuvijenga katika kata husika,kata ya Busunzu, Burungu, Budohoko na Kibondo Mjini inatakiwa angalau kuwa na vituo vya Afya kumi inasikitisha sana sijui itakapo fika 2020 mtaenda kuwambia nini Wananchi maana hakuna kitu kizuri mtakacho fanya kama kuwasaidia wananchi kuwaboreshea huduma za afya",alisema Bura.

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kibondo, Juma Mnwele alisema mpaka sasa wamepata milioni 500 kwaajili ya ukarabati wa zahanati ya Mabamba ilikuwa kituo cha Afya na kuwasaidia Wananchi wa Wilaya wanapata huduma ya Afya nzuri kama Serikali ya Awamu ya tano ilivyo kusudia kuboresha vituo vya Afya.

Aidha Mnwele aliwaomba madiwani kpamoja na wenyeviti wa kamati za maendeleo kuwashawishi wataalamu kufanya matumizi bora na uangalizi wa fedha za miradi ya Afya na kufuatilia kwa kufuatilia na kuthibiti ilikuzuia ubadhilifu kwa Watendaji wasio waaminifu kama kutajitokeza viashiria vya rushwa.

Aidha Mkurugenzi huyo alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Mgufuli jwa zawadi ya vifaa tiba pamoja na vitanda sita na magodaro yake vilivyotolewa katika hospitali ya Wilaya hiyo ,na kuipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa jitihada za kuboresha huduma ya Afya kwa kuwawezesha Wananchi kupata huduma stahiki na kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo.

No comments: