Mkuu
wa wilaya ya Busega, Tano Seif Mwera (kulia) akiwakaribisha wageni
kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania waliofika kijijini
Mwamanyili kujionea chanzo cha maji na eneo litakalotumika kwa ajili ya
kilimo cha umwagiliaji. Wageni hao waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya
(mbele kulia) akiwaongeza wageni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania kujionea chanzo cha maji kitakachotumika katika mradi wa
umwagiliaji wa Mwamanyili.
Mhandisi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Eng. Tumbu akitoa maelekezo kwa
ugeni kutoka TADB juu ya chanzo cha maji cha maji kitakachotumika katika
mradi wa umwagiliaji wa Mwamanyili.
Muonekano wa eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bibi Rosebud Kurwijila (aliyenyanyua mikono) akihimiza jambo wakati
walipotembelea eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo
umwagiliaji wa Mwamanyili.
Katika
kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuchochea mapinduzi ya
kilimo, Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB) imetembelea eneo utakaofanyika mradi wa kilimo cha kisasa cha
umwagiliaji la Mwamanyili Wilayani Busega mkoani Simiyu.
Akizungumza
lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa
la kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo ni kuunga mkono juhudi za serikali
katika kuwakwamua wakulima nchini kutoka katika kilimo cha kujikimu na
kwenda kwenye kilimo cha kibiashara ili waweze kujiongezea kipato.
Aliongeza
kuwa Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji ukianza kufanya kazi utatimiza
malengo hayo ya Benki kwani utasaidia kwa kiwango kikubwa katika
kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula
wakulima watakaolima katika skimu hiyo.
“Benki
ya Kilimo ipo tayari kuunga mkono miradi ya aina hii ambayo inalenga
katika kuendeleza miundombinu muhimu ikiwemo ya uendelezaji wa skimu za
umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji, pamoja na
masoko ili kumuongezea mkulima kipato,” alisema.
Kwa
mujibu wa mapendekezo ya mradi huo ambao unajumuisha zaidi ya ekari
2050, wananchi watakaolima katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa
misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya
jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha
ardhi.
No comments:
Post a Comment