Wednesday, November 8, 2017

BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’



Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Ebenezer Massawe (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipa nauli kielektroniki kupitia huduma mpya iliyozinduliwa na Kampuni hiyo ya 'Uhuru Pay' wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika leo jijiji Dar es salaam. Toka kushoto ni Afisa wa BCX Justin Lawena, Mkurugenzi Mtendaji wa wa BCX Seronga Wangwe, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.

Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Ebenezer Massawe (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipa nauli kielektroniki kupitia huduma mpya iliyozinduliwa na Kampuni hiyo ya 'Uhuru Pay' wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika leo jijiji Dar es salaam. Toka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BCX Tanzania, Seronga Wangwe, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.

Mkurugenzi Mtendaji wa wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Seronga Wangwe (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake kati ya Tegeta Nyuki na Kivukoni hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi kwa kukubali kutumia huduma mpya ya ‘Uhuru Pay’ kwa ajili ya malipo ya nauli kielektroniki wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia toka kushoto ni Afisa wa BCX, Justin Lawena, Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX), Ebenezer Massawe na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda


Mkurugenzi Mtendaji wa Business Connexion (BCX) Tanzania , Seronga Wange akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Mauzo na Masoko wa BCX, Ebenezer Massawe na kulia ni Afisa wa Kampuni hiyo, Justin Lawena.
Mkurugenzi Mtendaji wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Seronga Wange (kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.
Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda (kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Business Connexion (BCX) leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi na kulia ni Meneja Masoko na Mauzo BCX, Ebenezer Massawe.





Abiria wanaotumia usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam sasa hawatosumbuka tena kuhusu kutembea na fedha taslim mfukoni au usumbufu wa makondakta wa kutokua na chenchi, lakini pia wamiliki wa daladala wataanza kuona faida katika uwekezaji wao, kutoana na kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kukusanya nauli kielektroniki uliozinduliwa na Kampuni ya BCX chini ya bidhaa yake ya ‘Uhuru Pay’.

Tanzania inakuwa nchi ya nne Afrika kuzindua huduma hii baada ya Malawi, Zambia na Msumbiji ambako tayari imekwisha anza kutumika.

Mfumo huu wa ulipaji wa nauli kielektroniki una lengo la kurahisisha usafiri kwa watumiaji wa usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam kwa kuwapa fursa ya kulipia nauli kwa kutumia kadi. Kama mradi wa majaribio mfumo huu utaanzishwa kwanza kwenye ruti ya Tegeta Nyuki na Kivukoni kabla ya kuhamia kwenye maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BCX-Tanzania, Seronga Wangwe alisema ‘Uhuru Pay’ inalenga kurahisisha ulipaji wa nauli kwa wasafiri wa daladala na kuhakikisha kuwa abiria wanasafiri kwa utulivu na amani.

Tofauti na hilo ni kuwa wamiliki wa daladala wataweza kupata faida katika uwekezaji wanaofanya kwenye mabasi hayo kutokana na udhibiti na uwazi wa mapato yanayokusanywa”.

Aliongeza kuwa Abiria wa Daladala jijini Dar es salaam hawatakua na hofu tena ya kutembea na fedha taslim au usumbufu kutoka kwa Makondakta wa kutokuwa na chenchi, kwani kwa kupitia kadi ya Uhuru Pay watakuwa na Uhuru wa kupata huduma hiyo bila bugudha.

Urahisi huu utaambatana na ofa mbalimbali zitakazopatikana kwa abiria wote kama punguzo kubwa la bei za kusafiri na wakati mwingine kusafiri bure kabisa.

Seronga anaamini kuwa mfumo huu wa malipo kielektroniki utakubaliwa na Watanzania kwani tabia zao zinabadilika mara kwa mara na kukubali njia nyingine za malipo tofauti na fedha taslim. Hili ni jambo ambalo mataifa yaliyoendelea yamefanya kwa miaka mingi sasa, lakini mwenendo wa hivi karibuni wa malipo kupitia simu na matumizi ya kadi yanaonyesha kwamba kadi ya Uhuru Pay ni kitu ambacho Watanzania wanahitaji kwa sasa ili kuendana na mfumo wa maisha ya kisasa.

Kwa upande wake, Meneja Mauzo na Masoko wa BCX, Ebenezer Massawe alisema, mradi huo umekuwa katika matengenezo kwa muda mrefu sasa, na umepitia hatua mbalimbali za majaribio ili kuhakikisha kuwa vipengele vyote vinafanya kazi kama inavyohitajika.

“Mfumo huu tayari umeshafanyiwa majaribio ya kutosha na unazingatia kikamilifu sheria na kanuni zote, pamoja na mahitaji ya wahusika wanaohusika. Sasa tupo tayari kuingia kazini,” alisema Bw. Massawe.

Akielezea jinsi mfumo huu unavyofanya kazi, Massawe alisema kuwa mfumo huo wa kielektroniki utaunganishwa na wamiliki wa mabasi ili waweze kufuatilia moja kwa moja mauzo ya tiketi ya kila siku na kuongeza kuwa ndio ni kitu pekee ambacho wamiliki huwa wanakosa katika mfumo wa biashara ya leo.

Alisema abiria watakua na fursa ya kulipa kwa kutumia kadi ya Uhuru Pay ambayo itakuwa inapatikana katika vituo mbalimbali vya daladala, jijini Dar es Salaam.

Alielezea zaidi kuwa, Uhuru Pay ni bidhaa ya BCX, ambayo inatoa suluhisho kwa matatizo mbalimbali ya kifedha iliyoanzishwa na Kampuni ya BCX kwa wateja wake ili kupunguza mzigo wa usimamizi wa ukusanyaji wa fedha pamoja na uhamishaji wa fedha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

"Kwa sasa kadi ya Uhuru Pay itatumika kwa huduma za usafiri Daladala lakini baadae huduma zingine zaidi zitapatikana kwa kutumia kadi hiyo ikiwa ni pamoja na Malipo ya maduka makubwa katika, uwekaji gari mafuta, kutuma fedha kwa mitandao yote na akaunti za benki, malipo ya huduma kama LUKU, DAWASCO, NHC, AzamTV, ZUKU, Startimes, DSTV, nk "alisema.

Kwa Upande wake, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda alisema mfumo huo utaongeza makusanyo ya mapato kwa wamiliki wa daladala lakini pia mapato ya Serikali kwani wamiliki wa mabasi hayo watalazimika kulipa kodi kulingana na mauzo yao ya tiketi kwa siku.

"Serikali bado haikukusanyi mapato ya kutosha yanayotokana na huduma za usafiri, hivyo tumeamua kuunga mkono teknolojia hii mpya ili kuhakikisha kwamba Serikali inakusanya kodi ya kutosha," Kahetano, aliongeza kuwa mara baada ya mfumo huu kuwa rasmi basi madereva na makondakta watapata ajira rasmi”.

Aliongeza kuwa kupitia mfumo huu mpya, itakuwa rahisi kudhibiti suala la foleni kwenye ruti zinazotumia huduma hii kwa kuwa ni rahisi kujua njia ipi ina foleni na ipi haina.

Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa madaladala, Emmanuel Mlaponi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania alitoa wito kwa wamiliki kuiunga mkono huduma mpya ya 'Uhuru Pay' ikiwa kama watataka kudhibiti na kuongeza mapato ya biashara yai

No comments: