Tuesday, November 21, 2017

Airtel Money kugawa gawio la bilioni 2 kwa wateja

Wakati msimu wa sikukuu ya krismasi umewadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeupokea msimu huo kwa kuendelea kuwanufaisha wateja pamoja na mawakala wa huduma ya Airtel Money nchi nzima kwa kuwagawia gawio la shilingi bilioni 2 kutokana na utumia wao wa huduma ya Airtel Money 

Taarifa ilitolewa na kampuni hiyo leo ikiwa na kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso imethibitisha kuwa,

Gawio la faida kutokana na huduma ya Airtel Money hutolewa katika kila robo ya mwaka ambapo gawio la awali lilianza kutolewa Mwaka 2015, hadi kufikia leo hii jumla ya shilingi bilioni 11.8 zimeshagawiwa kwa wateja wa Airtel Money. Kila mteja wa Airtel Money hupata sehemu ya gawio hilo kulingana na salio linalosalia katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku.

“Tunapoingia katika shamrashamra za msimu wa sikukuu, Airtel tunatambua umuhimu wa kuwazawadia wateja wetu. katika msimu au wakati kama huu watu wengi hupanga ratiba za jinsi watakavyosherehekea kwa kupeana zawadi wakiwa na familia zao, tunafurahia kuona tuko katika wakati sahihi kwa kutoa gawio hili ili kutoa fursa kwa wateja wetu kuweza kutumia wakiwa na familia au wawapendao kwa kujipatia mahitaji yao muhimu ndani ya msimu wa sikukuu”.

Gawio hili la Airtel Money linaloaanza kutolewa leo linalotokana na faida iliyopatiikana kuanzia ya robo mwaka kuanzia mwezi Juni hadi Septemba 2017, ambapo watakaofaidika ni wateja wote wanaotumia huduma ya Airtel Money pamoja na mawakala wake nchini nzima. Tunajisikia furaha sana kugawa gawio hili ambapo kila mteja wa Airtel Money tapata na kisha mteja mweyewe ataamua kuitumia pesa yake atakavyo iwe kununua bando, muda wa maonge, kulipia LUKU au kufanya malipo ya bili za huduma mbalimbali” ilieleza taarifa hiyo

Airtel Tanzania itaenendelea na utekelezaji wa dhamira yake ya kutoa huduma za kifedha bora kwa njia ya mtandao ili kuongeza tija kwa watumiaji , unafuu na usalama wakati wowote. Huduma ya Airtel Money imekuwa na kuongeza watumiaji kutokana kuwa na umuhimu zaidi kwa wateja. Tunapenda kuwashauri wateja wa Airtel wot kutumia huduma hii ya Airtel Money kwa kukamilisha au kutimiza baadhi ya mahitaji yao ya huduma za kifedha ili kuwa sehemu ya gawio kama hili linayotolewa sasa” ilieleza taarifa hiyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu mgao wa gawio  la faida la bilioni 2 kwa wateja na watumiaji wa huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Isack Nchunda.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu gawio la bilioni 2 kwa wateja na watumiaji wa huduma ya Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano.

No comments: