Aliyasema hayo leo katika kikao cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo alisema watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka zaidi .
Licha ya hivyo lakini pia Waziri huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi .
Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja."Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya nchi na uzalendo "Alisema.
Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa
Aidha alisema kuwa mkakati wa shirika hilo ni kuhakikisha mpaka ifikapo 2020 madeni yote shirika hilo wanayoyadaiwa kwa wateja mbalimbali nchini yatakuwa yamekwisha kulipwa.
Sambamba na hayo alikema vitendo vya wizi wa umeme na kuwataka wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja na ambao watabainika watachukua hatua. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili kuwezesha
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani
Wajumbe na wadau mbalimbali wa nishati wakifuatilia kikao hicho leo
Baadhi ya wajumbe wa uongozi wa shirika kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uzalishaji Umeme Mhandisi Abdallah Ikwasa na kushoto ni Meneja wa Mwandamizi wa Tehama Dudu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanesco nchini Dkt Tito Mwinuka kushoto na Mkurugenzi wa REA Mhandisi Gisima Nyamuhanga wakifuatilia kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakimsikiliza kwa umakini Waziri Nishati,Dkt Medard Kalemani katika kikao hicho
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nishati ya umeme wa uhakika unapatikana.
No comments:
Post a Comment