Na Fredy Mgunda.
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.
akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi choo hiyo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa lengo ni kukikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati shule hiyo kutokana na miundombinu ya sasa si rafiki kwa wanafunzi.
"Maendeleo niliyopata mimi ni kutokana na kupata elimu katika shule ya Tosamaganga hivyo lazima tuikumbuke kwa kuendelea kuipatia msaada kadili tunavyoweza maana ukituangalia hapa unatuona wote tunavipato vizuri hivyo ni budi kukumbuka wapi tumetoka na tulikotoka kupoje tujia hivyo tutaithimini hii shule kila wakati kama tulivyofanya hivi sasa" alisema Mbilinyi
Mbilinyi aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.
“Leo nimerudi katika shule hii ya Tosamaganga kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi tumeanza kwa kujenga choo lakini changamoto bado zipo nyingi" alisema Mbilinyi
kwa upande wake mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa aliwataka wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya hiyo wawe vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali kurudisha fadhila katika shule hiyo.
"Nimekuwa nikipiga kelele muda mrefu kwenye vyombo vya habari muda mrefu juu ya kuzijali hizi shule zilizotuletea mafanikio ila saizi naanza kuona matumaini ya wanafunzi wengi wanazikumbuka shule walizosoma hapo awali ni jambo kubwa na la faraja sana" alisema Masunya
Masunya alisema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.
“Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania” Alisema Masunya
Naye Wakili msomi Protas Ishengoma aliwaomba wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.
“Hebu angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule hii”.alisema Ishengoma
Shule ya Tosamaganga ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha sasa kwanini leo hii hawazi kumbuki.
katika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.
Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga Iringa Damas Mgimwa akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi wakati wa kukata utepe wa kufngua choo hicho
Mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakikagua ubora wa vyumba vya vyoo hivyo
Hili ndio jengo jipya la choo kipya kilichojengwa na Tosamaganga Alumni Association kwa gharama ya shilingi millioni 30
Hawa ni baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo.
1 comment:
Hongera sana kwa Alumnae wote wa Tosamaganga na HONGERA za kipekee sana kwa Kaka Danford Mbilinyi Mzee wa F - Coy ya Col Mray(RTD)..! Pamoja sana Bro and keep it up.!!
Post a Comment